Na Asha Mwakyonde, Dar es Salaam
MBUNGE wa Segerea (CCM), Bonnah Kamoli,amewataka wakazi wa Tabata wanaopisha ujenzi wa Mradi wa mabasi yaendayo haraka (BRT), awamu ya sita kuendeIea kuishi, kufanya shughuli zao hadi serikali itakapotangaza kuwalipa upya fidia ili kupisha mradi huo.
Wakazi hao wamekuwa wakisubiri kulipwa fidia ili kupisha ujenzi wa mradi huo kwa takriban miaka sita tangu walipotangaziwa kulipwa fidia hiyo ambapo wameonesha shangwe kufurahia jambo hilo.
Hayo ameyasema leo Julai 22,2024 katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Tabata amesema mradi huo utakapoanza baada ya a wakazi hao kulipwa fidia watapata barabara ya kisasa na kwamba itawarahisishia katika masuala ya uchumi kwa kuwa hawatakuwa wakikaa muda mrefu kwenye foleni wanaopenda kufanya shughuli za kiuchumi.
Amesema mipango ya Serikali katika suala la miundombinu ya barabara wilaya ya Ilala ni kuboresha miundombinu hiyo kupitia Mradi wa Uendelezaji wa Jiji la Dar es Salaam (DMDP).
Mbunge Bonnah ameongeza kuwa mradi huo ukikamilika asilimia 80 ya kero zitakuwa zimetatuliwa.
"Naomba mkae katika maeneo yenu hadi Serikali itakapofika kuwalipa fidia ili kuweza kupisha upanuzi wa barabara ya mabasi yaendayo haraka," ameeleza mbunge huyo.
Aidha Bonnah ameipongeza Serikali ya Rais Dk.samia suluhu Hassan kwa utekelezaji wa Ilani ya CCM ikiwa ni pamoja na kuteleza miradi ya maendeleo ikiwemo sekta ya afya na sekta ya Elimu na Miundombinu ya Barabara.
Mmoja wa mkazi wa Mtaa wa Mtambani, Paul Abel, amesema kwa miaka Sita ameishi bila kukarabati nyumba yake jambo ambalo hakuweza kupata wapangaji.
"Wapangaji wamekimbia na hii imeniathiri kiuchumi, na kwa kauli hii ya mbunge wetu imerejesha uhai wa makazi yetu," amesema.
Akifunga mkutano huo mgeni rasmi Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya IIala, Said Sidde amesema kuwa chama hicho ni duka na kwamba wanawashukuru na kuwapongeza wauza duka hilo ambao ni viongozi wa kuona zile ahadi walizo ziahidi zinateketezwa zikiwamo za kutatua changamoto kwa wananchi.
"Kwenye Jimbo la segerea tumetekeleza baadhi ya ahadi za miundombinu kwenye kama ya barabarani, masoko na tunaowamba wananchi muwe na subiri kuhusu maji, mambo makubwa yamefanywa na serikali ya Rais Dk Samia," ameeleza Sidde.
Aidha amesema kuwa wanakwenda katika uchanguzi wa serikali za mitaa pamoja na ule Mkuu unaotaraajia kufanyika mwakani hivyo wananchi wajitokeze kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la mpiga kura
ili kuweza kupiga kwa lengo la kupata viongozi bora ambao watawaletea maendeleo wananchi hao.
Awali Naibu Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Ojambi Masaburi amesema Jambo la segerea ilani ya CCM imetekelezwa kwa kasi kubwa huku akimshukuru Rais Dk. Samia kwa fungua fursa za kiuchumi katika Jimbo hilo kwa kuboresha miundombinu ikiwamo ya barabara.
Amefafanua kuwa Halmashauri hiyo imekusanyasa bilioni 114.7 ambazo zitatumika kwa ajili ya miradi ya maendeleo.
0 Comments