BARABARA YA TABATA KISIWANI -MAWENZI KUJENGWA AGOSTI MWAKA HUU

Na Asha Mwakyonde, Dar es Salaam 

UJENZI wa barabara ya Tabata Kisiwani hadi Mawenzi yenye urefu wa kilomita 2.12 ambayo imeingizwa katika mpango wa Mradi wa Uendelezaji wa Jiji la Dar es Salaam (DMDP), unatarajiwa kuanza Agasti mwaka huu baada ya kuwalipa watu fidia wakazi wanaouzunguka mradi huo.

Akizungumza jijini hapa leo Julai 22,2024 katika ziara ya kukagua mirad ya mbunge wa Segerea Bonnah Kamoli, Mhandisi kutoka Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), Wilaya ya Ilala Mhandisi Legnard Mashanda amesema ujenzi huo wa mradi wa DMDP awamu ya pili upo katika hatua za mwisho kwa ajili ya kujengwa.

Mhandisi huyo amesema tayari zabuni imeshatangazwa na kwamba wapo katika uchambuzi wa mwisho ili kuweza kuanza utekekezaji.

Ameongeza kuwa wanatambua jambo la ulipaji fidia na kwamba suala hilo lipo kwa Mthaminishaji Mkuu wa serikali ambapo hivi karibuni wakazi hao wataanza kulipwa fidia ili kuweza kupisha mradi wa ujenzi.

"Tupo katika ziara na mbunge Bonnah kukagua Miradi na leo tupo katika barabara.Tunatambua changamoto katika miradi mikubwa inataratibu zake inafadhiliwa na benki ya dunia kuna jambo la kuwalipa watu fidia na kwa sasa tumefika hatua ya mwisho zabuni ilishatangazwa," ameeleza.

Mhandisi Mashanda amesema Mkandarasi atakuwa ataaza ujenzi, hatua za mwisho zilizopo ni za kusaini kataba baada ya watu kulipwa fidia zao. 

"Hatuwezi kumleta mkandarasi watu bado hawajapisha eneo la mradi, naomba matumaini ," amesema Mhandisi Mashanda.

Ameongeza kuwa barabara hiyo ujenzi wake unajumuisha kiwango cha zege kwa kuwa eneo la Tabata ni la maji maji na ni ya kudumu ambapo wataiwekea mirereji ya kisasa pamoja na taa za barabarani.

"Hili eneo la daraja hapa tunalifumua na kujenga jipya, hivyo changamoto ya barabara hii hadi Mawenzi itakuwa imetatuliwa," ameeleza.

Bonnah ameishukuru serikali ya Rais Dk Samia suluhu Hassan kwa jitihada kubwa za uwekezaji l kutatua changamoto katika maeneo ya a miundombinu ikiwamo ya barabara,maji na elimu.

Mmoja wa wakazi wa kisiwani Masoud Ally amesema kuwa mtaa huyo unwzungukwa na matatizo mengi huku akimshuru mbunge huyo kwa jitihada zake za kuhakikisha miundombinu inakuwa inaboreshwa.

Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI