Na Asha Mwakyonde,Dar es Salaam
CHUO cha Ustawi wa Jamii kimeanzisha kozi mpya ya malezi na makuzi ya mtoto ikiwa na lengo la kuleta tija kwa maendeleo ya watoto ambao utatolewa kwa ngazi ya Cheti na Diploma katika Kampasi ya Kisangara Mwanga Mkoani Kilimanjaro na kwamba kinaendelea na udahili.
Kozi hiyo inalenga kuwaandaa wakufunzi na wataalamu wa kwenda kufundisha walimu wa watoto, walezi wakiwemo wale wenye vituo vya kulelea watoto hao pamoja na vile vituo vya kutwa (Day care).
Akizungumza jijini Dar es Salaam kwenye banda lao katika maonesho ya 48 ya Kimataiafa ya Biashara Dar es Salaam (DITF),maarufu Saba Saba Mkuu wa chuo hicho Joyce Nyoni ameeleza kozi hiyo itakwenda kutoa suluhisho kwa kusaidia kuweza kuwajenga kwenye eneo la malezi na makuzi ya watoto.
Mkuu huyo wa Chuo ameongeza kuwa jamii inakabiliwa na changamoto kubwa katika suala malezi ambapo lionasababisha kutolea kwa ukatili wa watoto huku akiamini kwamba kozi hiyo inaenda kuleta tija ambapo wahitimu wataenda kuibadilisha jamii ya kitanzania juu ya malezi ya watoto.
Nyoni amesema kuwa kozi hiyo itakwenda kuwaongoza katika ulinzi wa mtoto, kuwafundisha taratibu za kuwaongoza katika michezo ya watoto, saikokojia ya mtoto, sanaa na vingine vingi vinavyohusu makuzi ya mtoto kwa ujumla.
Aidha amewataka Watanzania hasa vijana kuchangamkia fursa ya kujiunga na Chuo hicho kwa kuwa tayari kimeshaanza kufanya udahili.
0 Comments