TMDA YAENDELEA KUPAMBANA NA USUGU WA VIMELEA VYA DAWA, YATOA ELIMU SABA SABA


Na Asha Mwakyonde,Dar es Salaam 

MKURUGENZI Mkuu wa Mamalaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), Adam Fimbo ameeleza kuwa Usugu wa vimelea vya Dawa umekuwa ukiongezeka siku hadi siku kutokana na matumizi ambayo sio sahihi kwa baadhi ya watumiaji.

Pia imewataka wananchi kuendelea kuzingatia matumizi sahihi ya dawa na kuacha kutumia dawa kiholela bila kufuata maelekezo ya wataalamu.

Akizungumza jijini Dar es Salaam katika banda la Mamlaka hiyo kwenye Maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (DITF), maarufu Sabasaba amesema wanaendelea kuelimisha jamii dhidi ya mapambano ya usugu wa vimelea vya Dawa.

Mkurugenzi huyo amesema mamalaka hiyo katika kuhakikisha dawa zinatumika kwa ufasaha na usahihi wananchi wanapaswa kufuata maelekezo sahihi yanayotolewa na wataalam.

"TMDA tumeshiriki maonesho haya kwa lengo la kutoa elimu kwa wananchi juu ya matumizi sahihi ya dawa na kufahamu majukumu ya Taasisi hii," ameeleza Mkurugenzi Fimbo.

Mkurugenzi huyo ametoa wito kwa wananchi kuendelea kutembelea kwenye banda lao kupata elimu ya udhibiti na matumizi sahihi ya dawa awa na vitenganishi.

Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI