WAZIRI KAIRUKI APONGEZA ASKARI UHIFADHI TAWA KWA UTENDAJI MZURI


Na Mwandishi wetu 

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) amewapongeza Askari Uhifadhi kwa kazi nzuri huku akiwataka kuwa waadilifu. 

Ameyasema hayo leo Julai 8,2024 katika kikao na watumishi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA ) kilichofanyika Makao Makuu ya TAWA Mkoani Morogoro.

"Niwahakikishie kwamba Mheshimiwa Rais anatambua mchango wenu na kuwathamini sana, mnafanya kazi nzuri ya kupigiwa mfano " Mhe. Kairuki amesisitiza. 

Kufuatia hilo, Mhe. Kairuki ameelekeza TAWA kuangalia namna bora ya kupata Bima ya Maisha kwa Askari hao kwa kutambua mazingira ya hatari ya kazi zao.

Aidha, amewataka kuongeza kasi ya doria na operesheni kuhakikisha matukio ya ujangili wa Wanyamapori hayaongezeki.

Katika hatua nyingine Waziri Kairuki amewataka Askari hao kulipa kipaumbele suala la utatuzi wa migogoro ya mipaka kwa kuweka vigingi na alama zinazoonekana.

Ameipongeza TAWA kwa kuongeza makusanyo ya maduhuli na kuwasisitiza kuendelea na ujirani mwema kwa jamii sambamba na kutangaza vivutio vya utalii na kutoa elimu kwa umma.

Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI