PPRA: TAASISI NUNUZI 1,147 ZIMEJIANDIKISHA MFUMO WA NeSt

Na Asha Mwakyonde,Dar es Salaam 

MKURUGENZI wa Tafiti, Maendeleo na Ubunifu kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma nchini (PPRA),Mhandisi Masunya Nashon ameeleza kuwa taasisi nunuzi 1,147 tayari zimeshajiandikisha kwenye mfumo mpya wa ununuzi wa kielektroniki (NeST).

Pia amesema Serikali imekuwa ikijenga uwezo kwa taasisi nunuzi juu ya sheria mpya ,kanununi na mfumo wa ununuzi wa kielektroniki NeST na kwamba mafunzo yamefanyika katika Mikoa ya Mbeya Morogoro , Iringa na Mwanza ni kwa ajili ya Taasisi nunuzi na wafanyabiashara.

Akizungumza Julai 8,2024 kwenye Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam (DITF),maarufu Sabasaba, katila banda la Mamlaka hiyo Mhandisi 

Nashon amesema pamoja na wazabuni wazawa zaidi ya 22,000 kutoka makundi makuu matatu ambayo sheria mpya ya Mamlaka hiyo inataka yapate zabuni za serikali na kwamba idadi hiyo ya taasisi na wazabuni hao waliojiandikisha kwenye mfumo inaonesha mwitikio mzuri katika matumizi ya mfumo huo mpya.

Mhandisi huyo amesema Serikali imeongeza wigo ambapo kwa sasa zile zabuni zote za shilingi bilioni 50 kushuka chini ni lazima ziende kwa wazawa .

Mhandisi huyo ameongeza kuwa wanaona idadi ya wazabuni waliojiandikisha ni wengi na kwamba wanategemea kupata wazabuni zaidi kwenye maombi.

 "Ushindani unavyokuwa mpana na uwazi anayepata zabuni kwa hakika ni yule aliyekidhi vigezo vilivyowekwa ikiwa ni pamoja na kutumia Mfumo mpya wa NeST," amesema Mhandisi Nashon.

Aidha ametaja manufaa ya sheria mpya kuwa ni pamoja na kuongeza wigo wa maendeleo kwa wazawa ambao umegawanyika katika makundi Makuu matatu ,upendeleo kwa makundi maalum yaan vijana ,wanawake,wazee na watu wenye mahitaji maalum.

Mhandisi Nashon ameziasa taasisi nunuzi watangaze fursa hizo kwenye mfumo wa NeST wazabuni waingie kwenye mfumo ili waweze kuona hizo fursa na mchakato utaendelea kwenye mfumo na mwisho wa siku apatikane mzabuni.

Amefafanua kuwa Sheria mpya inaelekeza kila taasisi nunuzi serikalini kutenga asilimia 30 ya bajeti ya kuwezesha makundi hayo kushiriki katika makundi ya Serikali.

Mhandisi huyo ameongeza kuwa serikali kupitia Mamlaka hiyo imekuwa ikiendelea kutoa mafunzo kwa makundi maalum ambapo mwaka jana walikuwa na kampeni ya kuelezea fursa ambazo zipo katika ununuzi wa Umma.

Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI