Na Asha Mwakyonde,Dar es Salaam
MKURUGENZI wa Huduma za Ufundi kutoka Kampuni ya Ujenzi na Ukarabati wa Miundombinu ya Usafirishaji na Usambazaji wa Umeme (ETDCO), Dismas Massawe ameeleza kuwa mradi wa Mbeya ambao unaosimamiwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA), una jumla ya thamani ya bilioni 54 ambao wanaosambaza umeme katika vijiji 139.
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Julai 9,2024 katika banda la ETDCO kwenye maonesho ya 48, ya Kimataiafa ya Biashara Dar es Salaam (DITF),maarufu Saba Saba, amesema kuwa hadi sasa wamesambaza katika vijiji 130 na unatarajiwa kukamilika Julai mwishoni mwaka huu.
Mkurugenzi huyo amesema kuwa wamradi wa umeme Msomera ambao ni wa kujenga miundombinu ya usambazaji umeme katika nyumba 5000 ambazo zinajengwa na serikali na hadi sasa umesambaza katika nyumba 2500 za awali.
Ameongeza kuwa katika awamu ya kwanza ya mradi huo wanatarajia kukamilisha Julai mwishoni mwaka huu na kwamba nyumba 2500 zilizobaki ambazo zitajengwa kwenye eneo la Kilindi na Simanjiro unatarajiwa kukamilika ndani ya mwaka huu baada ya nyumba hizo kukamilika.
"ETDCO ni kampuni tanzu ambayo ipo chini ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), ilianzishwa mwaka 2016, lengo la kuanzishwa kwake ni kwa ajili ya kufanya kazi zote za kukarabati na ujenzi wa miundombinu ya usafirishaji na usambazaji wa umeme nchini," amesema.
Amesema kuwa kwa sasa kampuni hiyo inaendelea kufanya kazi zake katika mikoa mbalimbali nchini ambazo zipo chini ya TANESCO na kwamba wanafanya kazi za REA na zile wanazozipata kutoka kwa watu binafisi.
Naye Meneja wa fedha kutoka Kampuni hiyo CPA Sepetu Nyembo amesema kuwa kila mwaka mapato ya kambuni hiyo yamekuwa yakiongezeka.
"Mwaka wa fedha 2020/ 2022 kampuni ya ETDCO iliingiza jumla ya bilioni 48 kwa hesabu ambazo zimekaguliwa na mwaka wa fedha 2022/2023 ambao umeishia juni 30 imeingiza bilioni 64.5 na mwaka huu ambao umeisha juzi kampuni hii inatarajia kuwa na bilioni 90 lakini hesabu hii bado haijakagukiwa," ameeleza CPA Nyembo
CPA Nyembo amesema kuwa wao kama taasisi ya Umma wanakaguliwa na serikali, Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),
Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari Afrika Nashariki Staphane Nchimbi amewataka watanzania ambao wapo karibu na nguzo za umeme na hawajavuta umeme huo wavute kwa kuwa ETDCO kazi yake ni kuwahudumia watanzania hao.
Aidha ameipongeza serikali ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa jitihada kubwa ambazo zinafanya na serikali hiyo ya Uwekezaji katika miundombinu ya umeme huku akisema wao kama waandishi wa habari watakuwa pamoja Kampuni hiyo katika kuhakikisha wananchi wanapata taarifa sahihi juu ya kazi zinazofanywa na ETDCO.
0 Comments