Na Asha Mwakyonde,Dar es Salaam
SERIKALI kupitia Wizara ya Nishati imesema kuwa kazi kubwa inafanywa na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), katika maeneo mengi ambapo kuna nafasi ya kuendelea kuboresha kile kinachofanywa na Shirika hilo.
Hayo ameyasema jijini Dar es Salaam leo Julai 9,2024 na Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba, alipotembelea banda la TPDC katika maonesho ya 48 ya Kimataiafa ya Biashara Dar es Salaam (DITF),amesema wanataka Shirika hilo liwe na mchango mkubwa zaidi katika uchumi wa nchi.
Katibu huyo amesema eneo ambalo wanataka waongeze ushiriki wao katika uchumi ni eneo la gesi na kwamba gesi iliyopatikana nchini isambae kwa haraka zaidi kwenye vituo vya kujaza kwenye magari na isambae majumbani.
"Hii ni fursa kwenye maonesho kama haya kuufahamisha umma.
Tunataka kuona sekta binafsi inashirikishwa zaidi katika usambazaji wa gesi majumbani na gesi za kwenye magari,"amesema Mhandisi Mramba.
Ameongeza kuwa Waziri wa Nishati ambaye pia Naibu Waziri Mkuu Doto Biteko katika hotuba ya bajeti amesema wataongeza vituo vya gesi ya kujaza kwenye magari kwa kuanzia katika Jiji la Dar es Salaam ambapo hadi kufikia mwakani wanatarajia kuwa na vituo zaidi ya 30.
Mhandisi Mramba ameeleza kuwa hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu watakuwa wamejenga vituo Muhimbili, Kibaha, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Sinza, Mwenge, Goba, Mbezi Beach, Mbagala na kwamba baadhi vitajengwa na TPDC na vingine sekta binafsi.
"Hili la kuwa na kituo kimoja cha Ubungo Maziwa na Airport tutaachana nalo ndani ya mwaka huu na mwakani, tutakuwa na magari mengi yanazunguka ndani ya jiji wateja watafikiwa na kujaza gesi, hivyo suala la kujaza gesi kwenye magari tunajaribu kulirahisisha na kadiri inavyowezekana ili kuondoa adha ambayo wanayo," amesema.
Akizungumzia bomba la mafuta amesema mradi huo umefikia zaidi ya asilimia 30 na hadi sasa kilomita zaidi ya 600 za mabomba zimeshaingia nchini na kwamba wanatarajia kufikia mwishoni mwa mwaka 2025 utakuwa umekamilika.
Kwa mujibu wa Katibu mkuu huyo, Biteko katika hotuba ya bajeti alisema wataongeza vituo vya gesi ya kujaza kwenye magari kwa kuanzia katika Jiji la Dar es Salaam ambapo hadi kufikia mwakani wanatarajia kuwa na vituo zaidi ya 30.
Aidha amesema hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu watakuwa wamejenga vituo Muhimbili, Kibaha, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Sinza, Mwenge, Goba, Mbezi Beach, Mbagala na kwamba baadhi vitajengwa na TPDC na vingine sekta binafsi.
Hili la kuwa na kituo kimoja cha Ubungo Maziwa na Airport tutaachana nalo ndani yam waka huu na mwakani, tutakuwa na magari mengi yanazunguka ndani ya jiji wateja watafikiwa na kujaza gesi, kwahiyo suala la kujaza gesi kwenye magari tunajaribu kulirahisisha na kadiri inavyowezekana ili kuondoa adha ambayo wanayo.
Kuhusu bomba la mafuta amesema mradi huo umefikia zaidi ya asilimia 30 na hadi sasa kilomita zaidi ya 600 za mabomba zimeshaingia nchini na kwamba wanatarajia kufikia mwishoni mwa mwaka 2025 utakuwa umekamilika.
0 Comments