GCLA: TUNAFANYA UCHUNGUZI USALAMA WA CHAKULA KUMLINDA MLAJI

Na Asha Mwakyonde,Dar es Salaam 

KAIMU Mkurugenzi wa kurugenzi wa Bidhaa na Mazingira kutoka Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA), Shimo Peter amesema wanafanya uchunguzi wa vyakula mbalimbali pamoja na kuchunguza dawa ambazo zinakuwa katika makundi yote mawili za kisasa na zile za asili.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Julai 7, 2024 kwenye banda la GCLA katika moanesho ya 48 Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (DITF),maarufu Saba Saba ameeleza kuwa majukumu ya Mamlaka hiyo yamegawanyika katika makundi matatu.

Kaimu Mkurugenzi huyo amefafanua kuwa kundi la kwanza ni uchunguzi wa kimaabara ambayo inajihusisha na uchunguzi wa sampuli mbalimbali ambazo zinahusiana na bidhaa pamoja na mazingira.

Ameongeza kuwa wanafanya uchunguzi wa sampuli za mazingira na kwamba panapotokea uchunguzi wowote wa mazingira Mkemia Mkuu wa serikali anafanya shughuli hiyo.

Peter ameeleza kuwa kurugenzi hiyo wanafanya uchunguzi wa sampuli za usalama mahala pa kazi huku akisema inawezekana watu wanafanya shughuli zao katika mazingira ambayo yana athiri afya zao.

" Mamlaka hii ni moja ya maabara ambayo inashugulika na kufanya uchunguzi wa bidhaa hizi," ameeleza Kaimu Mkurugenzi huyo.

Akizungumzia dawa za asili amesema Mkemia Mkuu anafanya uchunguzi wa dawa hizo ili kuhakikisha zinakidhi viwango vya ubora wa Kitaifa.

" Pale mtanzania yoyote atakapotumia dawa hizi atapata huduma ambayo amekusudia na sio kuathirika hapo baadae, na kwa upande wa chakula tunaangalia usalama wa ubora wa vyakula na kuhakikisha vyakula vinavyoliwa vina kuwa na lishe iliyokusudiwa na vinakuwa salama kwa mtanzania yoyote ambacho atakula," amesema.

Amesema kwa upande wa pili wanaangalia kesi jinai ambapo wanakuwa na maabara moja ambayo inajihusisha na uchunguzi kwa mtu ambaye ameathirika na sumu.

Post a Comment

0 Comments

 KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA, KATIBA NA SHERIA YANOLEWA