KATI ya kesi 150 ambazo zilitoka Mahakama Kuu ya Dar es Salaam zilizopokelewa katika Kituo cha Usuluhishi 38 zilifanikiwa ambapo 97, hazikufanikiwa.
Akizungumza jijini hapa leo Julai 8,2024 katika maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam DITF maarufu Saba Saba kwenye banda la kituo hicho lilolopo katika kijiji cha Mahakama ya Tanzania, Hakimu Mkazi na Msaidizi wa Sheria wa Jaji, Rahel Kangagha amesema kuwa kesi hizo 150 kesi 66 zilitoka na 84 nilitoka Divisheni ya Ardhi.
Hakimu huyo ameeleza kuwa kituo hicho kinasikiliza migogoro yenye asili ya ya madai kwa kesi zinatoka Mahakama Kuu au Mahakama ya Divisheni ya Ardhi.
Akizungumzia faida za kutumia kituo hicho cha Usuluhishi amesema kinaokoa muda na kwamba wahusika wanapata muda mzuri wa kufanya shughuli zao za kiuchumi.
"Baada ya kesi kuleta katika kituo hiki wahusika ambao ni mdau na mdaiwa huitwa na kukaa kwenye meza ya mazungumzo ambapo wanapofikia muafaka na
wanasaini makubaliano endapo yatakiukwa na mdaiwa makubaliano haya yatatumika kukazia hukumu," ameeleza.
Aidha amewataka wananchi kubadilisha mtazamo kwa kutumia kituo cha usuluhishi zaidi badala ya Mahakama katika kusuluhisha migogoro ili kuokoa muda na kudumisha mahusiano katika jamii.
0 Comments