MWANAFUNZI UDOM ACHORA PICHA MOJA IKIMWELEZEA RAIS DK.SAMIA AKIWA KWENYE MAJUKUMU MATATU YA KITAIFA

Na Asha Mwakyonde, Dar es Salaam 

UBUNIFU wa uchoraji picha ya Rais Dk Samia Suluhu Hassan umekuwa kivutio katika moanesho ya 48 Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (DITF), maarufu Saba Saba ambapo watembeleaji wa moanesho hayo wamefurahishwa na picha hiyo.

Picha hiyo Dk.Samia Suluhu iliyochorwa na mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Chuo Kikuu cha Dodoma Enock Tarimo inamuelezea akiwa katika majukumu yake matatu makubwa ya Kitaifa.

Akizungumza na waandishi wa habari katika maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara jijini Dar Es Salaam Mkuu wa Idara ya Sanaa na Taaluma za Habari Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) Dk.Deograsia Ndunguru amesema,watu wengi wanaotembelea banda lao wamekuwa wakishangazwa na ubunifu na ujuzi ambao ametumia mwanafunzi wa mwaka wa kwanza fani ya sanaa chuoni hapo kuchora moja inayomuelezea Rais Dk.Samia akiwa katika mavazi matatu tofauti katika majukumu yake ya kitaifa.

Ameeleza kuwa wanafunzi wa fani hiyo Chuoni hapo wamekuwa wakifundishwa kutumia fursa mbalimbali kupitia rasilimali zinazowazunguka mazingira yao katika kujipatia kipato kwani sanaa ni ajira.

Dk. Ndunguru amefafanua kuwa Picha hiyo ni moja na inamuonesha Dk.Samia akiwa katika majukumu matatu tofauti.

"Ukisimama katikati anaonekana akiwa katika vazi la kiremba chekundu ambayo hutumika maeneo yote kwamba ni picha Rais, ukisimama kushoto anaonekana kama Mwenyekiti wa CCM akiwa katika vazi la kijani na nyeusi na ukisimama upande wa kulia anaonekana katika vazi la kijeshi kama Amiri Jeshi Mkuu ,kwa hizi ni ubunifu ambazo zinafanywa na wanafunzi wetu," amesema.

Ameeleza kuwa katika maonesho hayo wamekuja kuonesha shughuli mbalimbali zinazofanywa na chuo pamoja na wanafunzi na kwamba katika banda hilo kuna bunifu mbalimbali zilizofanywa na wanafunzi wao ikiwemo hiyo ,mapambo pamoja na picha nyingine nyingi zilizochorwa na wanafunzi hao.

Kwa upande wake Mhitimu wa UDOM 2023 Sultan Samwel ambaye amejiajiri katika kampuni yake ya mambo ya sanaa Talnis Creative Agency, ametembelea banda hilo na kufurahishwa kuona picha zake alizochora akiwa shuleni.

"Katika moja ya mitihani yangu nilizochora nikiwa chuoni pamoja picha za wanafunzi wenzangu, na nimeikuta hapa kwenye maonesho haya nimefurahi kuikuta, sanaa ni ajira kama zilivyofani nyingine kama vile ya daktari, sheria na nyingine nyingi,hivi sasa nimejiajiri katika kampuni yangu.

Vijana wanaopenda bunifu mbalimbali wametakiwa kufika katika banda hilo, kwenye chuo hicho baada ya maonesho hayo ili kujiunga na fani hiyo ambayo ni nyepesi ya kujiajiri.

Post a Comment

0 Comments

 KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA, KATIBA NA SHERIA YANOLEWA