WANANCHI WASHAURIWA KUTEMBELEA KIJIJI CHA TIRA SABA SABA

Na Asha Mwakyonde,Dar es Salaam 

MAMLAKA ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA), imewashauri wananchi Kutembelea kijiji cha bima kilichopo katika maonesho ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam (DITF), (Sabasaba),ili kusuluhisha changamoto za bima katika maonesho hayo.

Akizungumza jijini Dar es Salaam Julai 7, 2024 Msuluhishi wa Migogoro ya Bima kutoka TIRA , Margaret Mngumi amesema wanatatua migogoro ya bima kwa njia mbadala nje ya utaratibu wa kimahakama na kwa gharama nafuu na kwamba ndani ya kijiji hicho kuna banda la msuluhisi wa migogoro hiyo. 

Mngumi ameeleza kuwa wanatumia maonesho ya hayo kutoa elimu na kusuluhisha migogoro kutoka kwa wadau mbalimbali huku akiwataka wananchi kutembelea kijiji hicho ndani ya maonesho hayo ili kutatua migogoro yao.

“Migogoro tunayo isuluhishwa ni ile ya viwango vya fidia ya bima, eneo jingine la migogoro linatokana na tafsiri sahihi ya mkataba wa bima, mara nyingi mteja na kampuni ya bima wanakuwa hawaelewani juu ya tafsiri sahihi ya mkataba,” amesema Mngumi. 

Kwa upande wake Mwakilishi wa Kampuni za Bima zinazoshiriki maonesho hayo Alilya Kwayu, amewashauri Watanzania kujenga utamaduni wa kukata bima kama za afya, nyumba, magari, elimu, maisha ili iwe ziwasaidie pindi wanapopata majanga mbalimbali.

Naye Meneja Uandikishaji kutoka Kampuni ya Bima Mtawanyo (Grand Reinsurance), Charles Chanya, amesema wanatoa huduma kwa makampuni ya bima kwa lengo la kuyaongezea uwezo katika shughuli zao za kila siku. 

Ameongeza kuwa Kampuni za bima zinafanya biashara ambazo pengine inaweza kufikia hatua zinazidi uwezo na kwamba yanapozidiwa uwezo wanaenda katika kampuni za bima mtawanyo kuomba kuongezewa uwezo lengo likiwa ni kuandikisha bima zaidi.

Ameongeza kuwa wanaongeza uwezo wa kifedha huku akisema hawawapatii fedha, bali wanaandikisha bima kwa kutumia mtaji wao.

Post a Comment

0 Comments

 KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA, KATIBA NA SHERIA YANOLEWA