VETA YAMPONGEZA RAIS DK. SAMIA UWEKEZAJI UJENZI WA VYUO

Na Asha Mwakyonde, Dar es Salaam

MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), Anthony Kasore ameeleza kuwa lengo la serikali ya ya Rais Dk.Samia Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha kila eneo lenye wahitimu wa Mamlaka hiyo kunakuwa na nyenzo rahisi zinazoweza kutatua changamoto za jamii husika katika jamii.

Pia amempongeza juhudi za kujenga vyuo vingi vya VETA ambapo hadi kufikia 2025 kutakuwa na idadi ya vyuo takriban 145 vitakavyokuwa katika wilaya zote nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Julai 6,2024 katika maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) jijini Dar es Salaam kwenye Banda la VETA,Mkurugenzi huyo amesema kuwa mwaka 2022 walikuwa na vyuo vya VETA vipatavyo 29 ambavyo vilitoa huduma ambapo kwa sasa vipo 80 na ujenzi unaendelea wa vyuo 65 katika wilaya ifikapo 2025 vyuo vyote vitakuwa vimekamilika na kufanya idadi ya vyuo vya VETA kuwa takriban 145 ambapo kila wilaya itakuwa ina chuo hiki.

Mkurugenzi huyo, ameeleza kuwa hatua hiyo inakwenda kuleta tija katika uwekezaji ambapo wataalam katika fani mbalimbali wanakwenda kupatikana kupitia vyuo hivyo na kufanya kazi kwenye maeneo ya uwekezaji na viwanda.

"Mamlaka hii imekuwa ikitoa elimu ya ufundi kwa wenye ulemavu ambao nao wamekuwa karibuni nyenzo za kifundishia watu wenye ulemavu kutokana na changamoto za ufundishaji nanujifunzaji wanaouona wanapokuwa wanafundishwa na walimu wao," amesema.

Ameongeza kuwa Nia ya vyuo hivyo siyo kujenga tu ,bali ni kwa shughuli maalum ya kupata wataalam wenye ujuzi wa kutatua changamoto kwenye eneo husika kulingana na rasilimali zilizopo na mahitaji yake.

Post a Comment

0 Comments

MAJALIWA: MJI KONDOA TUMEKUSANYA ZAIDI YA MILIONI 126 KIPINDI CHA JULAI HADI JUNI MWAKA HUU