Na Asha Mwakyonde, Dar es Salaam
MAMLAKA ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA), imesema kuwa imetambulisha sheria mbili ambazo zinaenda kufanyiwa marekebisho ili kuwezesha utekelezaji wa sheria ya Mamlaka hiyo ambazo ni Sheria Sura Na.413 na sheria ya leseni za usafirishaji ya 1973 Sura Na.317.
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Julai 6,2024, Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Mwadawa Sultan katika jengo la LATRA kwenye maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam(DITF), amesema marekebisho hayo yamegusa maeneo mengi hususan katika eneo la usafirishaji watoto shuleni ambapo masuala yote ya mabasi ya shule yatahamishiwa katika kanuni nyingine.
Kaimu Mkurugenzi huyo wa huduma za sheria ameeleza kanuni ya usafirishaji sura Na 317 zipo kanuni mbili ambazo ni kanuni ya usafirishaji wa usafiri wa Umma ya 2020 na kanuni ambayo ipo katika leseni za usafirishaji sura Na.417.
Amesema, kanuni hizo zimefanyiwa marekebisho makubwa ikiwemo kutoa baadhi ya huduma zilizodhibitiwa chini ya kanuni hizi kwenda kwenye kanuni nyingine.
"Mfano usafirishaji wa watoto shuleni inaenda kwenye kanuni ya usafiri wa kukodisha ,lakini maboredho mengine ni namna ya kutoa adhabu ambazo sasa zitatolewa kulingana na ukubwa wa chombo na huduma ambayo mtu anafanya," amesema.
Ameongeza kuwa katika kanuni za usafirishaji Sura Na.417 na kanuni za usafirishaji mizigo nazo pia zilizotengenezwa 2020 na kwamba yapo maeneo yamerekebishwa kutokana na kero mbalimbali zilizokuwepo.
0 Comments