Rais wa Serikali ya Awamu ya Nne Dk. Jakaya Kikwete akisikiliza maelezo kutoka kwa afisa wa PURA, Ebeneza Mollel (kushoto), mara baada ya kutembelea banda la Mamlaka hiyo katika maonesho ya 48 ya Saba Saba yanayoendelea Jijini Dar es Salaam.
Na Asha Mwakyonde,Dar es Salaam
RAIS Mstaafu wa Serikali ya awamu ya nne Dk.Jakaya Kikwete amefurahishwa na mipango mizuri ya kunadi vitalu ya Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA),huku akihimiza kasi ya ufuatiliaji WA Mfuta ya Gesi Asilia nchini.
Pia ameitaka PURA kuhakikisha shughuli za utafutaji wa mafuta na gesi asilia nchini zinatekelezwa kwa kasi lengo likiwa ni kuongeza ugunduzi wa rasilimali hiyo muhimu.
Hayo ameyasema Julai 6, 2024 wakati alipotembelea banda la PURA katika maonesho ya 48 ya Kimataiafa ya Biashara Dar es Salaam (DITF), maarufu Saba Saba yanayoendelea Jijini Dar es Salaam.
"Nimefurahi kwa mipango mizuri iliyopo ya kunadi vitalu, jitihada za ziada zifanyike kuongeza kasi ili utafutaji wa gesi hii uongezeke," amesema Dk. Kikwete.
Aidha Dk. Kikwete ameongeza kuwa kasi ya utafutaji wa mafuta na gesi asilia nchini bado ni ndogo.
PURA kwa niaba ya Serikali imeendelea na maandalizi ya kunadi vitalu vilivyowazi vya utafutaji wa mafuta na gesi asilia nchini.
Miongoni mwa manufaa yatakayotokana na kunadi vitalu hivyo ni pamoja na kuvutia uwekezaji katika mkondo wa juu wa petroli utakaopelekea ongezeko la shughuli za utafutaji, uendelezaji na uzalishaji wa mafuta na gesi asilia nchini.
0 Comments