RAIS MSTAAFU DK. KIKWETE ATEMBELEA BANDA LA TANESCO, ASHAURI KUPUNGUZWA GHARAMA ZA UMEME

Na Asha Mwakyonde, Dar es Salaam 

RAIS Mstaafu Dk. Jakaya Kikwete. amelieleza Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), maadui wawili ambao ni kuni na mkaa kuwa wakipambana nao itasaidia kupatikana kwa watumiaji wengi wa nishati safi ya kupikia.

Pia ameeleza kuwa vita dhidi ya nishati safi ya kupikia nchini itafanikiwa endapo gharama ya umeme na gesi zitapungua.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Julai 6, 2024 alipotembelea maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (DITF), akiwa katika banda la TANESCO

“Mshindani wenu ni kuni na mkaa hivyo muongeze juhudi kuwaondoa kuchochea nishati safi, pia punguzeni gharama za umeme ili kila mtu aweze kumudu kwa sababu wengi hutumia kuni na mkaa kutokana na gharama ya umeme kuwa kubwa,” amesema Dk. Kikwete.

Aidha Dk. Kikwete ameuliza Shirika hilo kuwa linawashawishi vipi watu kununua majiko hayo ambayo hayatumii umeme mwingi ili yanunuliwe kwa wingi na waachane na mkaa?.

Post a Comment

0 Comments

 KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA, KATIBA NA SHERIA YANOLEWA