VETA YAUNGA MKONO JITIHADA ZA SERIKALI MATUMIZI YA NISHATI SAFI


Na Asha Mwakyonde,Dar es Salaam 

MAMLAKA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA),imeunga mkono jitihada za serikali katika utumiaji wa nishati mbadala kwa kuhakikisha vijana wao wanabuni mashine mbalimbali ambazo zinaweza kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi.

Akizungumza hayo Julai 6,2024 jijini Dar es Salaam wakati wa maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam ''Sabasaba'' Mwalimu wa VETA Chuo Dodoma,Yusuph Haule amesema VETA imetumia mkazo na nguvu kubwa katika kuona ni namna gani wataweza kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi katika kuhakikisha vijana wao wanaendana na teknolojia kwa kutengeneza au kubuni vitu ambavyo vitakuwa ni nyenzo za kupambana na mabadiliko ya tabianchi.

Amesema vijana wao wamekuwa wakitengeneza au kubuni mashine ambazo zinaendana na changamoto za uhitaji wa teknolojia na kusaidia kufikia makundi ambayo yanahitaji kufikia teknolojia.

''Kwa mwaka huu,Chuo cha VETA Dodoma,tumekuja na ubunifu wa mashine inayoweza kudhibiti magugu ambayo inatumia nishati ya umeme wa jua na sio genereta ambayo inachangia uchafuzi wa mazingira,''amesema Haule.

Kwa upande wake Mhitimu wa Chuo hicho Dodoma Veta ,Patrick Ezekiel amesema mashine waliyobuni inadhibiti magugu kwa kukataa nyasi ngumu,laini na pia inajembe la kufanyia parizi katika eneo la bustani.

"Tumeandaa mashine hii kwaajili ya kumsaidia mkulima kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kwa kuwa kifaa hiki hakitumia mafuta wala haitoi moshi ni rafiki wa mazingira,''amesema na kuongeza

'' Mashine hii haina gharama kubwa kwa mkulima maana haitumii mafuta wala kuichajisha katika umeme wa majumbani bali inajiendesha kwa umeme wa jua(solar) na kuifanya system ya mashine kufanya kazi kwa kiwango kikubwa,''amesema.

Amesema mashine nyingi za parizi zinatumia injini na zinazalisha moshi kwa kiwango kikubwa na pia zinakelele hivyo zinampa changamoto kubwa mkulima pindi anapokuwa anafanya shughuli zake.

Post a Comment

0 Comments

 KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA, KATIBA NA SHERIA YANOLEWA