RAIS DK.SAMIA KUTUMIA USAFIRI WA TRENI YA MWENDOKASI AGOSTI MOSI


 Na Asha Mwakyonde,Dodoma

RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan anatarajia kuzindua treni ya mwendokasi ambapo atasafiri na treni hiyo kutokea mkoani Dar es Salaam hadi mkoani Dodoma ambako uzinduzi huo utafanyika .

Akizungumza jijini hapa leo Julai 30,2024, na waandishi wa habari kuhusu uzinduzi huo ,Mkuu wa mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule amewaasa wananchi wa mkoa huo na wale wa mikoa ya jirani kuhudhuria uzinduzi huo ili kujionea na kumuunga mkono Rais dk.Samia kwa juhudi zake za kukamilisha kipande hicho cha Dar es Salaam -Morogoro-Dodoma.

Amesema kufuatia uzinduzi huo Tanzania inaenda kuandika historia mpya ya kuwa na treni ya mwendokasi miongoni mwa nchi chache Afrika.

"Tunaenda kuandika historia ambayo haitajirudia maana treni ya mwendokasi ndiyo inaanza ,kwa hiyo tuna kila sababu ya kumpongeza Rais Dkt.Samia kwa juhudi zake za kuifaharisha Dodoma na Tanzania kwa ujumla."amesema Senyamule

Ameongeza kuwa kazi ya Serikali ni kutengeneza mazingira mazuri ya wananchi kufanya maendeleo huku akisema treni ya mwendokasi inaenda kuleta maendeleo ya wananchi.

"Leo Dk.Samia amekamilisha relo ya mwendokasi (SGR) kwa ajili ya maendeleo ya wananchi na Taifa kwa ujumla."amesisitiza.

Wakati huo Senyamule amegawa 'reflector' kikoti cha waendesha boda boda na bajaji wa stesheni ya mwendokasi ambao ndiyo watakaotumika kubeba abiria watakaoshuka kwenye treni ya mwendokasi kuelekea majumbani kwao.

Ameeleza kuwa hiyo ni kwa ajili ya usalama wa abiria ambao wamefurahia safari ya treni hiyo na kuhakikisha wanafuka majumbani kwao salama.

"Ninyi mmewekwa hapa kwa ajili ya kuhakikisha sasa abiria yule ambaye amesafiri na treni ya mwendokasi na amefurahia safari,tunataka akifika hapa akipanda bodaboda au bajaji aendelee kufurahia safari na kufika nyumbani salama.

Mkuu wa Mkoa huyo ametumia nafasi hiyo kuwaasa madereva hao kutumia vizuri fursa waliyoipata kwa kufanya kazi hiyo kwa weledi,uaminifu na utulivu huku wakiwa nadhifu na wenye kupendeza.

 Aidha amewataka madereva hao kuwa mabalozi wazuri wataokaizungumzia Dodoma vizuri kwa wageni ambao wanafika Dodoma kwa mara ya kwanza.

Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI