Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi (Mb) (kulia) akipokea nyaraka mbalimbali za utendaji kazi kutoka kwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana (Mb) (kushoto) wakati wa makabidhiano ya Ofisi yaliyofanyika Ofisi za Wizara Mtumba, jijini Dodoma, Agosti 20, 2024.
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi (Mb.) akisaini kitabu mara baada ya kuwasili Ofisi za Wizara Mtumba, jijini Dodoma kwa ajili ya hafla ya makabidhiano ya Ofisi Agosti 20 2024.
Naibu Waziri Wizara ya Katiba na Sheria Mhe. Jumanne Sagini (wa kwanza kulia) akiwa pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara Bw. Eliakim Maswi (wa kwanza kushoto) wamewaongoza Watumishi wa Wizara ya Katiba na Sheria katika mapokezi ya Naibu Katibu Mkuu mpya wa Wizara hiyo Dkt. Franklin Rwezimula Agosti 20,2024 katika Ofisi za Wizara Mtumba, jijini Dodoma.
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi (Mb) (kulia) akiwa na Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana (Mb) (kushoto)wakisaini nyaraka za makabidhiano ya ofisi katika Ofisi za Wizara ya Katiba na Sheria leo Agosti 20,2024 Mtumba jijini Dodoma.
Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi (Mb) akizungumza na Watumishi wa Wizara ya Katiba na Sheria (hawapo pichani) wakati wa hafla makabidhiano ya Ofisi iliyofanyika katika Ofisi za Wizara Mtumba, jijini Dodoma Agosti 20,2024.
Na Hyasinta Kissima – WyKS
WAZIRI wa Katiba na Sheria Mhe.Prof. Palamagamba Kabudi (Mb) ameanza kazi rasmi kwa kuwataka Watumishi wa Wizara hiyo kuwa kinara katika kutekeleza kwa vitendo falsafa ya 4R ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Prof. Kabudi ameyasema hayo tarehe 20 Agosti 2024, wakati akizungumza na Watumishi katika hafla fupi ya makabidhiano ya Ofisi yaliyofanyika Ofisi za Wizara Mtumba jijini Dodoma.
"Tunapozungumzia Reconciliation hatuangalii makundi ya Kisiasa pekee. Wapo Wakulima na Wafugaji ambao nao wanahitaji upatanisho.Yapo mambo ya kijamii,uchumi, utamaduni ambayo yanahitaji upatanisho.Tunapokwenda kutoa Msaada wa Kisheria tunapatanisha watu, tunafanya usuluhishi, tunasaidia watu kuelewa haki zao.Tunafanya Reform katika Sheria mbalimbali.
Aidha, Waziri Kabudi amesema kuwa anamshukuru sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kumwamini ambapo ameahidi kufanya kazi kwa bidii na kwa uaminifu.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi ofisi, Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye ndiye aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana alisema Wizara ya Katiba na Sheria ilimpatia ushirikiano wa kutosha katika kuhakikisha anatimiza majukumu yake ipasavyo na kuwataka watumishi waendeleze mshikamano huo kwa Prof. Kabudi ambaye hii ni mara yake ya tatu kuongoza wizara hii.
Kwa upande wake Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amewashukuru Watumishi wa Wizara ya Katiba na Sheria kwa ushirikiano waliompatia katika kipindi chote na amesema kuwa katika Wizara ya Maliasili na Utalii Maliasili yapo maeneo mengi ambayo Wizara hiyo inashirikiana na Wizara ya Katiba na Sheria hususani katika kusimamia Haki za Binadamu.
0 Comments