TRA NANE NANE DODOMA YAWAKUMBUSHA WAFANYABIASHARA KULIPA KODI


 Na Asha Mwakyonde, DODOMA 

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA), imewakubusha wafanyabiashara kulipa kodi ambapo kwa mujibu wa Sheria kila mfanyabishara mwenye mauzo ya milioni 11 kwa mwaka anapaswa na mashine za kutolea risiti (EFDs).

Pia inawakaribisha wale wote ambao hawana namba ya utambulisho ya mlipa kodi (TIN NUMBER), kutembelea banda la TRA katika maonesho ya Nane nane kitaifa yanayofanyika katika viwanja vya Nzuguni kwa ajili ya kupata namba hiyo ambayo inatolewa bila malipo.

Akizungumza jijini hapa leo Agosti 2,2024 katika maonesho hayo Afisa Msimamizi Kodi Mwandamizi Philip Eliamini amesema kuwa mteja anatakiwa kuwa na namba ya kitambulisho cha Taifa ( NIDA), na kwamba katika banda hilo huduma nyingine inayopatikana ni makadirio ya kodi.

Afisa huyo ameeleza kuwa kwa mfanyabishara ambaye bado hajakadiriwa katika mwaka huu wa fedha hasa kwa wakazi wa Dodoma huduma hiyo inatolewa kwenye banda la mamalaka hiyo.

"Tunatoa rai kwa wananchi wote wa Dodoma na kwa wale ambao hawana namba ya utambulisho ya mlipa kodi (TIN NUMBER), kutembelea banda letu la TRA kwa ajili ya kupata namba hii aje na Namba yake ya Namba ya Kitambulisho cha Taifa (NIDA), na inapatikana bila malipo," amesema.

Amefafanua kuwa kwa wale wanaodaiwa kodi na wanahidaji namba za malipo zinapatikana katika banda hilo huku akisema kuna wasambazaji wa mashine za kutolea risiti (EFDs),na kwamba kuna wataalam wanaitoa elimu za mashine hizo.

"Na wanaohitaji mashine hizi zinapatikana katika banda letu la TRA nawakumusha tu kwa mujibu wa Sheria kila mfanyabishara mwenye mauzo ya milioni 11 kwa mwaka anapaswa kuwa mashine hizi," ameeleza.

Ameongeza kuwa katika maonesho hayo wanapata fursa ya kujenga mahusiano mazuri na wadau wao walipa kodi na wengine.

Katika hatua nyingine ameeleza kuwa Mamlaka hiyo inatoa msamaha wa kodi kwa zana za kilimo zikiwamo pembejeo mbalimbali za kilimo.

Aidha amesisitiza kuwa msamaha wa kodi hautolewi kwa mkulima mmoja bali kwenye zana zinazotumika kwa wakulima.

"Tunamshukuru Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Profesa Riziki Shemdoe kwa kutembelea banda letu na kuchukua maoni mazuri amewashauri wote wanaonufaika na misamaha hii ya kodi kuwasilisha nyaraka mapema.

Amesema kuwa kwa mujibu wa Prof. Shemdoe wanaoagiza zana hizo wahakikishe wanawasilisha nyaraka mapema katika ofisi za mamalaka hiyo badala ya kusubiri zifike.

Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI