INADES KUKUTANISHA WADAU WA MIFUGO KESHO KUJADILI HALI YA MNYAMA KAZI PUNDA, PROF. SHEMDOE KUWA MGENI RASMI


Na Asha Mwakyonde, Dodoma 

WADAU wa mifugo wanatarajia kukutana kesho katika mdahalo wa kujadili tafiti ambazo zimefanywa na wataalam waliopewa kazi na Taasisi isiyo ya kiserikali ya Inades-Formation Tanzania (IF TZ), ambayo inayofadhiliwa na Brooke East Africa baada ya serikali kusitisha uchinjaji wa mnyama kazi punda hapa nchini ambapo katika mdahalo huo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Profesa Riziki Shemdoe.

Akizungumza jijini Dodoma leo Septemba 24, 2024 Mkurugenzi Mtendaji wa IF TZ Mbarwa Kivuyo, amefafanua kuwa walipeleka wataalam hao katika maeneo matatu ambayo ni kuangalia hali ikoje tangu serikali ilivyopiga marufuku biashara ya uchinjaji wa mnyama kazi punda.

Mkurugenzi huyo ameyataja maeneo mengine kuwa ni kuangalia Sheria ya mifugo inasemaje kuhusu mnyama huyo na kupitia mitaala ya vyuo vya mifugo kuanzia ngazi ya Shahada na Astashahada endapo masuala ya punda yameingizwa kwenye mitaala yao.

" Wanavyuo wanaozalishwa na vyuo hiyo ndio wanaenda kuhudumia mifugo na wanapoenda katika maeneo yao ya kazi mnyama punda hahesabiki kwa kuwa hawajafundishwa, tumeona tuangalie maeneo haya kujua hali ikoje kwa mnyama huyu," ameeleza Kivuyo.

Awali Afisa Miradi masuala ya mifugo kutoka Taasisi hiyo George Pharles amezitaja baadhi ya shughuli kuu za Inades ni kuboresha huduma za matibabu kwa wanyama kazi punda ikiwa ni pamoja na kuwezesha jamii kuwa na kiliniki za matibabu hayo kwa mnyama huyo, mafunzo maalum kwa watoa huduma za afya ya mifugo, kwa wauza dawa katika maduka ya dawa za mifugo pamoja na usimamizi kuweza kuhudumia wanyama.

Amesema shughuli nyingine ni usimamizi wa vikundi vya wamiliki na watumia punda, kuwezeaha na kuimarisha vikundi hivyo kwa wanyama hao, mafunzo ya huduma, haki ustawi wa wanyama kazi punda , kuwezesha na kuboresha kipato kwa watumiaji na wamiliki wa punda hao.

Afisa Miradi huyo ameongeza nyingine ni utetezi wa ustawi wa haki za mnyama huyo ikiwa ni pamoja na kushiriki katika uhamasishaji wa uundwaji wa sera bora za kumlinda mnyama kazi punda, kushiriki katika tathimini, tafiti na kuendesha programu shuleni kwa lengo la kuhamasisha ustawi wa haki za mnyama kazi punda.

Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI