SERIKALI kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kushirikiana na Sekta binafsi inaendelea kutoa elimu na kuhamasisha jamii juu ya umuhimu wa kumhifadhi mnyama kazi punda na kuzuia biashara haramu ya nyama na ngozi za punda.
Hayo yamesemwa leo Septemba 26,2024 jijina na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dk.Edwin Mhede katika kikao cha wadau cha kuangalia matokeo ya tathimini 3 zilizofanyika chini ya
Shirika lisilo la kiserikali ya Inades-Formation Tanzania (IF TZ), inayofadhiliwa na Brooke East Africa baada ya serikali kusitisha uchinjaji wa mnyama huyo hapa nchini amesema mnyama kazi Punda ana faida zaidi akiwa hai kuliko akiwa amekufa.
Amesema kuwa Serikali inayoongozwa na Daktari Samia Suluhu Hassan inachukulia suala hilo kwa uzito na imeshachukua hatua na kuhakikisha punda wanahifadhiwa na kudhibiti biashara haramu inayowalenga Wanyama hao.
Ameeleza kuwa wadau wa Sekta binafsi wameendelea kufanya kazi kwa karibu na Serikali na Mashirika ya Kimataifa na Asasi za Kiraia zinazojishughulisha na masuala ya Ustawi wa Wanyama, kuhakikisha kwamba biashara ya nyama na ngozi za punda inakomeshwa.
"Napenda kuchukua fursa hii kulipongeza sana shirika la INADES Formation Tanzania kwa kushirikiana na wadau wengine wa ustawi wa Wanyama Tanzania kufanya tathimini ya hali ya ustawi wa mnyama kazi Punda hapa Nchin," ameeleza.
Naibu Katibu Mkuu huyo amesema kiwa jitihada hizo zinazofanywa, hazitoshelezi bila ushirikiano wa wadau huku akitoa wito na kuwasihi wadau wote kuunga mkono juhudi zinazofanywa na kushirikiana katika kumlinda punda na kudhibiti biashara haramu ya ngozi na nyama za punda nchini.
Mkurugenzi Msaidizi kutoka Wizara ya Uvuvi wa Mifugo anayeshughulikia Ustawi wa Wanyama Dk.Annette Kitambi amesema serikali imekuwa ikitoa elimu ya ustawi wa mnyama punda kupitia vyombo vya habari,uteuzi wa wakaguzi wa masuala ya ustawi wa wanyama katika mamlaka za serikali za nitaa na uteuzi wa bodi ya kumshauri waziri masuala ya ustawi wa wanyama nchini.
"Awali Mkurugenzi wa Shirika la IFTz, Mbarwa Kivuyo, amesema mradi wa kuboresha ustawi wa mnyama kazi punda ambao unatekelezwa katika mikoa ya Dodoma, Iringa na Singida umeanza kutekelezwa 2019.
Kivuyo ameeleza kuwa tangu umeanza kutekelezwa kumekuwa na matokeo chanya kwa kufanikisha kusitisha biashara ya punda ambayo ilishamiri sana hapa nchini kuanzia 2014 hadi 2022 hali iliyokuwa inahatarisha kupotea kwa mnyama huyo.
0 Comments