DIWANI SAMBALA: SUALA LA WANAFUNZI KULA SHULENI SI LA HIARI

Na mwandishi wetu,Chemba Dodoma 

DIWANI wa Kata ya Mondo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba, Said Sambala amesema kuwa suala la wanafunzi kula chakula shuleni si jambo la hiari bali ni la lazima kwani linatokana na Mwongozo wa Serikali juu ya Mpango wa Lishe Mashuleni uliotolewa na Serikali.  

Kauli hiyo ameitoa Oktoba 12, 2024 wakati akitoa salamu za serikali katika Mahafali ya 27 ya Shule ya Sekondari ya Mondo iliyopo Wilayani humo ameeleza kuwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan amekuwa akitoa fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya huduma za jamii katika kata hiyo na hivyo wananchi hawanabudi kuunga mkono juhudi hizo kwa kuhimiza watoto kwenda shuleni bila kukosa huku wakiwapatia mahitaji ya msingi yakiwemo chakula. 

" Mheshimiwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ametoa zaidi ya Shilingi Bilioni Moja na Milioni Miatatu kwenye Kata yetu ya Mondo kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya huduma za jamii ikiwemo elimu" amesema.

Sambala na kuongeza Rais Dk. Samia ametuongeza Shilingi Milioni mia moja kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Waida.

Diwani huyo amesema juhudi za Rais Dk. Samia zinapaswa kuungwa mkono na wananchi kwa kuwapatia watoto chakula shuleni ilikuondoa tatizo la utoro lililokithiri.

 "Nadhani Kuna haja ya Bodi ya Shule tukutane haraka kulipatia ufumbuzi changamoto hii ya utoro. Kusema kweli tafsiri yake ni kwamba mahala fulani jamii yetu hatuko sawa," amesema Sambala.

Hata hivyo Diwani Sambala ametumia fursa hiyo kuwahimiza wananchi wa Kata ya Mondo pamoja na Wilaya ya Chemba kujitokeza kwenye zoezi za kujiandikisha kwenye daftari la wakazi ili kupata sifa ya kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa unatarajiwa kufanyika tarehe 27 Novemba mwaka huu. 

"Niwaomba wananchi wa Mondo na Wilaya ya Chemba kwa ujumla tuhimizane kujiandikisha kwenye daftari la la wakazi ilitupate sifa ya kupiga kura kuwa chagua viongozi bora kwa kipindi cha miaka mitano mingine," ameeleza Sambala.

Wakati huo huo Mwenyekiti wa Bodi ya Shule hiyo Thomas Chorray akimkaribisha Mgeni Rasmi Mkuu wa Idara ya Mipango ya Mazingira Profesa Fadhil Hamza Mgumia wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijiji ameunga mkono kauli ya diwani Sambala huku akisema wao kama wazazi wataenda shambani kubeba chakula na wanafunzi tunapaswa kuwapatia chakula.

Aidha ameeleza kuwa wanafunzi hao wakisoma na kupata chakula ni dhahiri watafaulu na kwamba hiyo itapungiza utoro shuleni.

Kwa mujibu wa risala iliyosomwa na wahitimu wa kidato cha Nne wa Shule hiyo Maria Zeno na Hussein Maloko mbele ya Mgeni Rasmi Prof. Mgumia wamesema kuwa jumla ya wahitimu 122 kati yao wavulana 54 na wasichana ni 68 wamehitimu na kwamba kati ya wanafunzi 225 wavulana wakiwa 90 na wasichana 135 na kufanya wanafunzi 103 wavulana 36 na wasichana 67 hakumaliza masomo kwa sababu mbalimbali ikiwemo utoro. 

Post a Comment

0 Comments

MAJALIWA: MJI KONDOA TUMEKUSANYA ZAIDI YA MILIONI 126 KIPINDI CHA JULAI HADI JUNI MWAKA HUU