Viwanja vya EPZA-Geita
MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT ) Mary Chatanda (MCC) ameeleza kuwa Sekta ya Madini imestawi kwa kiasi kikubwa chini ya Uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan.
Aidha, Chatanda ameeleza kuwa Rais Dk.Samia amewezesha kuongezeka kwa kasi ya ukuaji wa sekta ya Madini ikiwemo ushirikishwaji na uwezeshwaji wa Wanawake ikiwa ni pamoja kupatiwa leseni na mitaji inayowawezesha kujiinua kiuchumi.
Hayo ameabinisha leo Oktoba 12,2024 alipotembelea Mabanda mbalimbali ya washiriki wa Maonesho ya Saba ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini yanayofanyika katika Viwanja vya EPZA Bomba mbili Mkoani Geita.
"Tumejionea namna gani maelekezo ya Rais wetu Dk.Samia yanatekelezwa, tumeona vikundi mbalimbali vya Vijana na Wanawake ambao wamewezesha kupatiwa mitaji na leseni kuweza kufanya shughuli zao" amesema Mwenyekiti Chatanda na kuongeza.
"Hakika hatuna budi kumshukuru Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan ambae anawapenda wananchi wake,anataka kila mwananchi awezeshwe kiuchumi,"amesema
#uwtimara
#jeshiladktsamiadktmwinyi
#Kaziiendelee
#ushindinilazima
#mitanotena
0 Comments