MAKATIBU WAKUU NA WADAU WA TANZANIA SAFARI CHANNEL WAKUTANA DODOMA


Na Mwandishi wetu,Dodoma 

Kamati ya Makatibu Wakuu wa Wizara mbalimbali pamoja na wadau wa televisheni ya Tanzania Safari Channel wamekutana kuzungumzia uendeshaji wa Chaneli ya Utalii ya Tanzania Safari Channel inayomilikiwa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC).

Akizungumza mara baada ya Kikao cha Makatibu Wakuu wa Wizara Wadau wa Tanzania Safari Channel kilichofanyika katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Centre jijini Dodoma Mwenyekiti wa Kikao hicho ambaye pia ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu, Dkt. Jim Yonazi Makatibu Wakuu hao wamekutana kwa lengo la Kupokea na Kujadili taarifa ya kikao cha Wakuu wa taasisi.

Dkt. Yonazi ipo haja ya yakuendelea kuboresha chaneli hiyo ili iendelee kuwa bora na kuwavutia watazamaji wa makundi yote ndani na nje ya Nchi.

Ameongeza kuwa chaneli hiyo itakuwa yakuigwa barani Afrika ambayo itaitangaza Afrika kutokea Tanzania.

Pamoja na hayo kikao hicho kimejadili mikakati mbalimbali ya kuiwezesha chaneli hiyo kuendelea kuendesha shughuli zake za uzalishaji wa vipindi vya utalii vyenye maudhui ya ubunifu zaidi.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa ameeleza kuwa wizara yake katika kuisimamia TBC inayo dhima ya kuhakikisha kuwa tija ya chaneli hiyo inapatikana na changamoto zote zinatatuliwa ili jamii iweze kunufaika na uwepo wa chaneli hiyo kwa kushirikiana na Wizara ya Maliasili na Utalii.

Naye Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Bi. Fatma Hamad Rajab ameishauri TBC kufanya kazi kwa ukaribu na Kamisheni ya Utalii Zanzibar ili kutangaza vivutio vingi vya utalii vilivyopo Zanzibar.

Post a Comment

0 Comments

TAARIFA ZA WASTAAFU NHIF KUHAKIKIWA MAHALI WALIPO