MWAKAGENDA AHOJI UWEKEZAJI WA MAZAO YA PARACHICHI NA CHAI KUKOSA SOKO, WAZIRI MKUU AELEZA MKAKATI WA SERIKALI


Na Asha Mwakyonde, DODOMA 

MBUNGE Viti Maalum Mkoa wa Mbeya Sophia Mwakagenda juzi ameuliza swali bungeni jijini Dodoma katika maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambapo alitaka kujua kwa nini Serikali isitoe agizo kwa wawekezaji wanaonunua mazao ya Parachichi na Chai waweze kuyanunua kwa wakati badala ya kuacha mpaka yaharibike.

Mwakagenda ambaye pia alihoji "kumekuwa na baadhi ya mazao yakipata bei nzuri na yakisaidia wakulima kupata mahitaji ,lakini kunekuwa na mwenendo mbaya kwa wawekezaji na baadhi ya wanunuzi hawafanyi vizuri kwa wakulima hasa yale mazao yanayoharibikia shambani,

“Ni nini mkakati wa Serikali kusema na kutoa agizo kwa wawekezaji na baadhi ya wanunuzi kuhakikisha wananunua mazao hayo kwa wakati ikiwemo parachichi na chai kwani wamekuwa wakichelewa kwa makusudi ili bei iweze kushuka kwani hapo wakulima wanakaribia kupata hasara.?”alihoji Mwakagenda

Mbunge huyo alihoji ni nini mkakati wa Serikali kutoa agizo kwa wawekezaji na baadhi ya wanunuzi ni kuhakikisha wananunua mazao hayo yakiwamo parachichi na chai ambapo wamekuwa wakichelewa kwa makusudi ili bei iweze kushuka ndipo wakulima wanakaribia kupata hasara.?.

Akijibu swali hilo leo Februari 6,2025 Waziri Mkuu Majaliwa amesema kuwa serikali imejipanga kuhamasisha uwekezaji kwenye viwanda kwa ajili ya uchakataji wa mazao ya wakulima hususan yale yanayoharibika haraka Ili wakulima hao wasipate hasara.

Amesema kuwa kumekuwa na baadhi ya mazao yakipata bei nzuri na yakisaidia wakulima kupata mahitaji huku akisema kumekuwa na mwenendo mbaya kwa wawekezaji na baadhi ya wanunuzi.

Waziri Mkuu ameeleza wawekezaji hao hawafanyi vizuri kwa wakulima hasa yale mazao yanayoharibikia shambani.

Waziri Mkuu Majaliwa amesema Serikali imejikita katika kusimamia kilimo nchini, kilimo ambacho kinatoa mazao ya biashara na chakula na manufaa na sasa inaenda kujikita katika uchakataji ili kilimo kiwe na tija.

Amesema katika usimamizi huo wa mazao ya biashara Serikali inatambua kwamba zipo changamoto ikiwemo mazao mengine yanayoharibika kwa haraka na hivyo kuuzwa kwa bei ya chini.

“Mkakati wa Serikali ni kwamba tutahakikisha mazao haya tunayawekea utaratibu ambao ndani ya Serikali tumeamua kuweka Mamlaka / Bodi zinazosimamia mazao kuanzia uratibu tangu kwenye Kilimo," ameeleza.

Amesema lengo la mkakati huo ni kuokoa mazao hayo ambayo wamehamasisha uwekezaji kwenye viwanda ili waweze kuchakata mazao haya kwa ili yasifikie hatua ya kuharibika.

Waziri huyo ameeleza kuwa kwa kuchakata mazao hayo watapata bei nzuri na kwamba mkulima anapata mazao mengi.

Amefafanua kuwa hatua hiyo imelenga kuokoa mazao hayo yanayoharibika kwa haraka mashambani kusababisha wakulima kupata hasara.

Post a Comment

0 Comments

TAARIFA ZA WASTAAFU NHIF KUHAKIKIWA MAHALI WALIPO