Dodoma
BAADA ya kuidhinishiwa jumla ya Sh trilioni 2.44 katika mwaka wa fedha 2025/2026, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imeanza rasmi mchakato wa kuwasilisha bajeti yake mpya kwa mwaka 2026/2027, huku wadau na wananchi wakisubiri kwa hamu mwelekeo na vipaumbele vipya vitakavyochochea maendeleo ya sekta hiyo muhimu nchini.
Leo Mei 06, 2026, Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Wanu Hafidhi Ameir, amewasilisha Bungeni jijini Dodoma randama za makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo, ikiwa ni hatua ya awali kuelekea hotuba rasmi ya bajeti inayotarajiwa kuwasilishwa kesho Mei 07, 2026.
Katika mwaka wa fedha uliopita, Wizara hiyo iliomba na kuidhinishiwa Sh trilioni 2.44 kwa ajili ya utekelezaji wa majukumu yake, hali inayoongeza hamu na matarajio ya wengi kuona ni kwa kiwango gani bajeti ijayo itaongeza nguvu katika kuboresha elimu, sayansi na teknolojia nchini.

0 Comments