MBUNGE AHOJI LINI KITUO CHA AFYA UPUGE KITAPATIWA GARI LA WAGONJWA


Na Asha Mwakyonde, DODOMA 

MBUNGE wa Tabora Kaskazini Athumani Maige leo Februari 11,2025, bungeni jijini Dodoma katika swali lake la msingi amehoji je, lini Serikali itakipatia gari la Wagonjwa Kituo cha Afya cha Upuge - Uyui.?

Akijibu swali hilo Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI),Dk.Festo Dugange amesema kuwa Serikali imeendelea kuimarisha huduma za rufaa za wagonjwa ambapo katika kipindi cha mwaka 2021/2022 hadi 2024/2025, Serikali imenunua na kusambaza magari 382 ya kubebea wagonjwa kwenye halmashauri kwa kuzingatia mahitaji, ambapo kila jimbo limepokea angalau gari moja la kubebea wagonjwa. 

Amesema Halmashauri ya Uyui ilipokea magari matatu ya kubebea wagonjwa ambayo yamepangwa kutoa huduma katika Hospitali ya Wilaya, Kituo cha Afya Igalula na Loya. 

Naibu Waziri huyo aidha aliongeza Kituo cha Afya Upuge - Uyui kina gari la wagojwa ambalo ni chakavu hali inayopelekea kuhitaji matengenezo ya mara kwa mara.

Amesema,Serikali inaendelea na utekelezaji wa mpango wa manunuzi wa magari ya wagonjwa na kuyapeleka kwenye vituo vyenye uhitaji zaidi kikiwemo Kituo cha Afya cha Upuge Uyui.

Mbunge huyo akiuliza swali la nyongeza alisema "Kituo cha Afya cha Upuge Uyui Hakijapata kuwa na gari la wagonjwa kulikuwa na gari bovu la Halmashauri na liliengeshwa pale na kituo kile kina hudumia kata tatu je serikali ipo tayari kutambua kwamba kituo hakina gari la wagonjwa linalofanya kazi?

"Kwa vile kituo Cha afya Cha upuge kinahudumia watu zaidi ya 30,000 na hakina huduma ya X-ray wala Ultrasound vinapatika katika hospitali ya Wilaya ambayo ni kilomita 35 kutoka pale je serikali ipo tayari kupeleka gari la wagonjwa sasa katika mgao unaendelea? alihoji.

Akijibu maswali hayo Naibu Waziri huyo alieleza kuwa"Mheshimiwa Maige amekuwa akifuatilia mara kadha na kuhitaji gari la wagonjwa katika kituo cha afya cha Upuge na mimi mara kadhaa tumekaa nae tumekubaliana nikuhakikishie mheshimiwa mbunge tayari tumeshaingiza katika orodha ya vituo vya afya ambavyo vimepewa kipaumbele kutapatiwa gari mojawapo ni kituo cha Upuge".

Aidha amemhakikishia mbunge huyo kwamba hatua za utekelezaji zinaendelea huku akisema serikali imeweka mpango wa kukamilisha majengo ya huduma, kuweka vifaa tiba muhimu na kusogeza huduma za afya karibu na wananchi 

"Nimhakikishie Mheshimiwa kwamba katika kipindi hiki Cha miaka mitatu serikali imenunua digital X-ray zaidi ya 250 na kusambaza kwenye vituo vya afya na katika hospitali za Halmashauri,"amesema.

Ameongeza kuwa kituo hicho alichokitaja mbunge kitapewa kipaumbele ili kipate mashine ya digital X-ray kwa lengo la kusogeza huduma karibu zaidi na wananchi.

Post a Comment

0 Comments

KIGOMA YAPATA MWAROBAINI WA UKATILI WA KIJINSIA