MTEMVU AHOJI UTOFAUFAUTI KAYA MASIKINI MJINI NA VIJIJINI GHARAMA ZA KUUNGANISHIWA UMEME

Na Asha Mwakyonde, DODOMA 

MBUNGE wa Kibamba Issa Mtemvu leo Februari,11,2025 bungeni jijini Dodoma ameuliza swali la msingi kwamba Je,Serikali inatofautishaje Kaya maskini Vijijini na Mijini katika kuwaunganishia umeme nchini.

Akiibu swali hilo Naibu Waziri wa Nishati Judith Kapinga ameeleza kuwa Serikali kupitia Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imeweka mwongozo wa gharama za kuunganisha umeme kwa wateja, ambapo gharama hizo hutofautiana kulingana na hali ya eneo.

Kapinga amesema kuwa kulingana na mwongozo huo, maeneo yanayotambuliwa kama miji na vijiji miji, gharama ya kuunganisha umeme ni shilingo 320,960 na kwa maeneo ya vijiji gharama ya kuunganisha umeme ni shilingi 27,000.

Akiuliza maswali mawili ya nyongeza mbunge alihoji "Je serikali haioni kutofautisha watu masikini wa mjini na Vijijini ni kutokuwapatia haki masikini katika fursa ya kujiinua kiuchumi kujipatia Nishati ya umeme?

"Kwa kuwa masikini hawa katika pande zote za mijini na Vijijini wanatambuliwa wakiwa katika Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) serikali inatumia fedha nyingi kuwalipa je serikali hamuoni kupitia TASAF inaendelee kuwapa ile haki ya upatikanaji wa Nishati ya umeme kwa kutumia shilingi 27,000 kiwaunganishia umeme hawa wananchi wanaoishi kwenye miji? alihoji mbunge huyo.

Akijibu maswali hayo Naibu Waziri huyo amesema "Nashukuru kwa maswali mawili ya mbunge na naomba niyajibu kwa pamoja,Mheshimiwa Mwenyekiti miradi ya kupelekwa umeme inatekelezwa kulingana na upatikanaji wa fedha katika aina( Categories),tofauti tofauti.

Naibu Waziri Kapinga amefafanua kuwa miradi ambayo wanaipeleka kwa shilingi 27,000 ni ile ambayo imegawanywa, (Categories), kwa miradi ya Vijijini ambayo serikali imeweka ruzuku ili wananchi hao waweze kupata umeme kwa gharama nafuu kidogo .

Amesema kuwa kwa maeneo ya miji na vijiji miji wanayo miradi mingine ambayo wanawasaidia wananchi ambao uwezo wao wa kuunganisha umeme ni kidogo na kwamba lazima waunganishiwe katika kipindi ambacho miradi hiyo inatekelezwa.

Ameeleza kuwa katika maeneo ya miji wanaipeleka miradi hiyo hususani yale ya pembezoni ili wananchi waweze kupata umeme kwa gharama ambayo ni himilivu kidogo.

Naibu Waziri huyo amemhakikishia mbunge huyo kwamba miradi hiyo wanaitekekeza kwa aina tofauti tofauti kulingana na maeneo ili kuendeIea kumpa hueni mwananchi katika kuunganisha umeme.

Post a Comment

0 Comments

MBUNGE AHOJI LINI KITUO CHA AFYA UPUGE KITAPATIWA GARI LA WAGONJWA