📍Wadau waombwa kutia nguvu kuuboresha, utasaidia kupunguza kelele za wapangaji.
Na Asha Mwakyonde
MBUNIFU na Mwalimu kutoka Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), Mkoa wa Pwani Hamis Salum ameomba wadau kujitokeza kuwasaidia ili kuweza kukamilisha mfumo wa mita ya maji ambayo inatuma taarifa moja kwa moja katika mfumo huo.
Akizungumza leo Juni 30,2025. katika maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam 2025, ‘Saba Saba’ amesema kuwa mita hiyo ni tofauti na mita nyingine zilizozoeleka nyumbani ambazo hadi uisome kwa kuiona katika eneo ulipo.
Salum ameeleza kuwa mita hiyo imekuja kutatua matatizo mawili ambayo ni ya taarifa kufika kwa wakati na tatizo la wateja wengi kutumia mita moja huku akitolea mfano katika nyumba za wapangaji.
Ameongeza kuwa matarajio yao ni kuuendeleza mfumo huo kuwa kamili ili uanze kutumika kwa jamii.
"Nyumba za kupangisha wapangaji wakiwa 10 au 20 kupitia mfumo huu watatumia mita moja na kila mtu atakuwa na kadi yake tofauti na zile ambazo zinatumika majumbani kwa sasa ," amesema.
Amesema kupitia mfumo huo inahitajika mita mita moja huku akifafanua kuwa mfumo unatenganisha matumizi ya wapangaji hao kwa kutumia kadi.
"Kadi hizi tumezisajli na kila mpangaji atakuwa na kadi yake kila mtu na matumizi yake," ameeleza.
Amefafanua kuwa mfumo huo ni tofauti na mita zilizozoeleka nyumbani ambazo hadi uisome kwa kuliona katika eneo ulipo.
0 Comments