📍Lengo ni kuwasaidia wajasiriamali kujiinua kiuchumi
Na Asha Mwakyonde, DODOMA
WAJASIRIAMALI wadogo na kati wanahitaji nguvu zaidi kutoka taasisi za kifedha ili waweze kufanikiwa na kuweza kukuza uchumi wao pamoja na Pato la Taifa kwa ujumla.
Safari ya ujasiriamali imejaa changamoto nyingi zinazoweza kuathiri ukuaji wa biashara zao pamoja na kuathiri ndoto za kufikia malengo kutokana na changamoto za kifedha.
Upatikanaji wa mikopo ni mgumu kutokana na masharti magumu ya benki na taasisi za kifedha, ambazo mara nyingi huhitaji dhamana kubwa kutoka kwa wajasiriamali mbalimbali.
Mfuko wa Self MF imejikita katika kutoa mikopo kwa wajasiriamali ambao wanafanya shughuli zao kihalali kwa lengo la kuhakikisha nchi inaongeza Pato lake kupitia Kodi za wajasiriamali hao.
Akizungumzia mfuko huo namna unavyotoa mikopo kwa wajasiriamali Meneja wa Mfuko wa Self MF Kanda ya Kati Dodoma na Singida Aristid Tesha, anasema kwa sasa mfuko huo umeanzisha bidhaa mpya ambapo wanatoa mikopo kwa wajasiriamali wanaojihusisha na Nishati mbadala,Nishati safi wanajikita katika kuuza bidhaa za gesi na vifaa vyake.
Anaongeza kuwa wanaangalia kwa waliojikita kwenye mambo ya vifaa vya umeme wanazitumia kama Nishati mbadala.
Anasema hiyo yote ni nia ya serikali ya kumfanya Mtanzania apunguze matumizi ya mkaa,kuni katika eneo linalomzunguka.
"Hawa wanaofanya Nishati mbadala tumewalenga na tunawapa mkopo wenye riba nafuu ili waweze kupanua wigo kufanya shughuli zao na kuweza kuwafikia wananchi," anaeleza.
Tesha anasema wanawawezesha wajasiriamali hao ili waweze kushirikiana na serikali katika kupunguza matumizi ya kuni na mkaa.
Anafafanua kuwa kwenye Nishati mbadala wamejikita kwa wanaosambaza sola za umeme waliopo vijijini na mijini wanaowauzia wananchi kwa bei nafuu.
Aidha akizungumzia mikopo ya watumishi wa Umma alisema kuwa wanatoa mikopo kwa watumishi kupitia mishahara yao ambapo huduma ya mikopo hiyo inapatikana katika matawi yaliyopo mikoa 12.
MIKOPO YA KILIMO
Akizungumzia mikopo kilimo kwa wajasiriamali ambao wanafanya shughuli za kilimo anaeleza kuwa kumekuwa na changamoto kubwa ya kupata dhamana kwa ajili ya mikopo hiyo.
Meneja hiyo anasema wameingia ubia na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB),kwa ajili ya kutoa dhamana kwa wale ambao wamepungukiwa dhamana pindi wanapofika katika mfuko huo kuomba mikopo hiyo ili waweze kutimiza malengo yao.
"Benki ya kilimo TADB wamekuja kwetu na mkulima anapokuwa kwetu au asasai ya inayojishughulisha na kilimo tutampa muongozo namna nzuri ya kupata mkopo huu wa kilimo pamoja na muongozo wa kupata dhamana kutoka TADB," anasema.
Anafafanua kuwa Self MF wanatoa mikopo kwa wajasiriamali ambao wanafanya shughuli za kiuchumi kwenye mikoa 12 na vituo viwili kwa ajili ya kutolea huduma.
Tesha anaongeza kuwa wajasiriamali hao wanaweza kupata mikopo yenye riba nafuu na kuweza kufanya shughuli zao kiuchumi bila kujali matabaka ilimradi shughuli zinazofanywa na mjasiriamali ziwe za halali na iwe inamuingizia kipato katika jamii inayomzunguka.
Aidha anaeleza kuwa mfuko huo unatoa mikopo kwa watumishi na kwamba inapatikana katika ofisi zao zote katika matawi yote yaliyopo 12 nchini.
Naye Meneja Rasilimaliwatu na Utawala Johari Magara anaeleza kuwa lengo kuu la kushiriki maadhimisho hayo ni kuwapa huduma wananchi ya kuwapa taarifa ya huduma za mikopo zinatolewa na mfuko huo.
Anaeleza kuwa mfuko wa self MF ulianza rasmi 2014 ambapo lengo kuu ni kuwawezesha wananchi kiuchumi kwa kuwapatia mikopo yenye unafaa.
"Mikopo ya Self MF ya aina mbalimbali ikiwemo mikopo ya watumishi wa Umma, wafanyabisahara, wajasiriamali wadogo na wa kati, mikopo ya wakulima, mkopo wa wazabuni pamoja na Nishati safi," anasema.
Anaeleza kuwa mbali na mikopo hiyo pia mfuko huo unatoa mkopo wa bima za gari,nyumba, za wizi na nyingine zote.
ELIMU YA FEDHA
Meneja huyo anaeleza kuwa mfuko huo una dhima kuu ya kutoa elimu katika masuala ya fedha kwa wananchi wote kwa wanaofika katika ofisi za Self MF kwa lengo la kupata mikopo.
"Pia huwa tunawaalika wananchi katika makundi ili kuwapatia elimu hii ya fedha," anabainisha Magara.
TAKWIMU
Akizungumzia takwimu anasema kuwa takwimu za miaka minne kuanzia 2021 hadi 2024 mfuko wa self MF ulitoa mikopo kwa wananchi yenye thamani ya shilingi bilioni 162.3.
Meneja hiyo anasema Self MF imeweza kuhudumia wateja wake 127,000 ikiwa ni idadi ya mikopo 9853 na kwamba mfuko huo umeweza kuwahudumia wateja wa bima jumla 7442.
"Mfuko wa Self MF una vituo viwili na matawi 12, licha ya kuwa na matawi haya mfuko una toa huduma nchi nzima haka kama sehumu haina matawi tuna. waafikia wananchi wote wenye uhitaji wa mikopo," anaeleza idadi hiyo meneja huyo.
Anayataja matawi hayo kuwa ni Dar es Salaam, Tanga, Morogoro, Mtwara, Dodoma, Kahama,Geita, Mwanza, Iringa ,Mbeya na Arusha.
Meneja huyo anawakaribisha wananchi kwenda kupata huduma zilizo thabiti katika mfuko huo kama ilivyo kwa taasisi nyingine za serikali.
Anasema kuwa mfuko wa self MF unachangia kuwainnua wananchi kiuchumi kutokana na mikopo inayotolewa ambayo ni ya chini ya wajasiriamali wadogo.
"Mjasiriamali mdogo tuna mkaribisha ambapo anatueleza vizuri biashara,shughuli ambayo anayoifanya katika ukuuzajii, kujjieenndesha kibiashara ambapo tuna mshauri namna ya kujiendesha na baadae kumpatia mkopo," anasema.
Anasema wananchi wote wa Tanzania wenye kipato cha chini na kuuendelea mfuko huo unawawezesha na kwamba waanafursa ya kupata mikopo.
0 Comments