MASWI AKUTANA NA WAJUMBE WA AFRIKA WA UANGALIZI WA UCHAGUZI MKUU


Dar es Salaam 

KATIBU Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Eliakim Chacha Maswi amekutana na ujumbe wa waangalizi wa uchaguzi Mkuu kutoka Umoja wa Afrika (African Union Election Observation Mission) jijini Dar es salaam, tarehe 27 Oktoba mwaka huu. 

Ujumbe huo wenye waangalizi 72 kutoka nchi 31 za Afrika umeongozwa na mwenyekiti wao ambae ni Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Botswana, Mhe. Mokgweetsi Eric Keabetswe Masisi. 

Aidha Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilitoa mwaliko kwa ujumbe huo ili kuangalia na kushauri kuhusu hali ya uchaguzi katika hatua ya maandalizi, wakati wa uchaguzi na baada ya uchaguzi.

Katika Majadiliano yao waangalizi hao walijikita katika nafasi ya Wizara ya Katiba na Sheria kwenye uchaguzi mkuu.






Post a Comment

0 Comments

MASWI AKUTANA NA WAJUMBE WA AFRIKA WA UANGALIZI WA UCHAGUZI MKUU