Dar es salaam
WIZARA ya Nishati imeendelea kutoa elimu ya Nishati Safi ya Kupikia kwa makundi mbalimbali katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara (SABASABA) yanayoendelea katika Viwanja vya Mwl. Nyerere jijini Da es Salaam.
Wanafunzi kutoka Shule ya Sekondari ya St. Maximilian jijini Dar s Salaam ni sehemu ya wanafunzi waliopata elimu hiyo baada ya kutembelea banda la Wizara ya Nishati.
Wanafunzi hao baada ya kupata elimu ya nishati safi ya kupikia, wamepatiwa madaftari yenye ujumbe wa nishati safi ya kupikia kwa lengo la kuendelea kufikisha elimu hiyo kwa makundi mengine.



0 Comments