Songea, Ruvuma
NAIBU Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb), leo Julai 3, 2026, amewasili katika Uwanja wa Ndege wa Songea mkoani Ruvuma kwa ajili ya kushiriki Kongamano la Wanawake lililoandaliwa na Rizex For Life Foundation, lenye jina la "Mtoko wa Familia."
Mhe. Mahundi, amepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Brigedia Jenerali Ahmed Abbas, pamoja na viongozi wengine wa Serikali.
Kongamano hilo linatarajiwa kufanyika Julai 4, 2026 mkoani Ruvuma na litawakutanisha wanawake wa Ruvuma, viongozi mbalimbali wa Serikali, pamoja na wasanii, kwa lengo la kujadili masuala yanayohusu ustawi wa familia, uwezeshaji wa wanawake na maendeleo ya jamii.











0 Comments