WAZIRI MKUU MAJALIWA AIFAGILIA BENKI YA STANBIC KWA KUSHUSHA RIBA ZA MIKOPO


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati akifungua  Kongamano la Sita la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi jijini Dodoma, Septemba 19, 2022. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) .

Baadhi ya washiriki wa Kongamano la Sita la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati akifungua kongamano la sita la Uwezeshaji Wananchi jijini Dodoma, Septemba 19, 2022. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

NA ASHA MWAKYONDE, DODOMA

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amezita taasisi za kibenki kuimarisha huduma zake na kuhakikisha zinatoa mikopo kwa riba nafuu kama ilivyofanya Benki ya Stanbic ambayo imeanza kupunguza riba zake kutoka asilimia 15 hadi 12.5. ili watu wengi wapate mitaji ya kufanya biashara.

Hayo ameyasema jijini hapa Septemba 19, wakati akifungua na baadae kuzindua Utekelezaji wa Sera ya Uwezweshaji Wananchi Kiuchumi katika Kongamano la sita la Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), lenye  kauli mbinu isemayo " Uwezeshaji Wananchi katika Uwekezaji" amesema taasisi hizo za kifedha ziendelee kutoa huduma na kuhakikisha wanufaika wake wanufaike kwa mikopo yenye riba nafuu.

" Stanbic mmeanza kupunguza riba kutoka asilimia 15 hadi 12.5  nawapongeza na natamani kuona mnashusha hadi kufikia 'single digital' lakini pia bado ipo chini Ila mnaweza kushusha ikawa 9,8 na 7, ili watu wengi wapate mitaji wafanyie kazi mitaji ile na waweze kurudisha kwa uhakika pia  taasisi za fedha mliopo hapa mlione hili," amesema Waziri Mkuu.

Aidha Waziri huyo ameeleza kuwa anatamani ifikapo mwakani katika Kongamano hilo kusikia viwango vya riba vimeshuka huku akizitaka taasisi hizo kuendelea kuwa karibu na wananchi katika kuwafikishia huduma pamoja na kuwafungulia akaunti.

Ameongeza kuwa Benki nyingine hazijafika wilayani hivyo wanapaswa kujitangaza zaidi na kwenda kufungua matawi katika wilaya hizo anbazo haina huduma za kifedha.

Akimkaribisha Waziri Mkuu, Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Ashatu Kijaji amesema kuwa Kongamano hilo limelenga kuwawezesha wadau kuelewa dhana ya uwezweshaji wananchi Kiuchumi.

Awali Mwenyekiti wa NEEC, Prof. Aurelia Kamuzora amesema kuwa ukosefu wa mitaji mikubwa ni changamoto kwa wazawa hali inayosababisha kuachia fursa kubwa  za utekelezaji wa miradi mikubwa kuchukuliwa na wageni hivyo kushindwa kushindana kwenye zabuni zenye miradi hiyo.

Akimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya  Stanbic Tanzania Limited  Kevin Wingfield, Mkuu wa Kitengo cha Biashara  Kai Mollel amesema Kongamano hilo ni chachu ya kuwezesha ushiriki wa Watanzania katika miradi ya kimkakati na uwekezaji unaofanyika hapa nchini  (Local Content).

Ameongeza kuwa wao kama benki wanaamini uchumi wa nchini unaendeshwa na wafanyabiashara wadogo na wakati pamoja na wajasirimali huku akitolea mfano ushirikiano waliouanzisha na NEEC, katika program iitwayo ' Supplier Development Program' ambayo inalenga kutoa ujuzi na utaalamu, masoko na mitaji  ili wafanyabiashara hao waweze kuzitambua, kuzifikia na kufanufaika na fursa za uwekezaji nchini hasa katika miradi ya kimkakati.

Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI