Mgombea ajinadi kuwa anaweza kuliongeza Bunge


Aliyekuwa mgombea nafasi ya Ubunge Jimbo la Chato mwaka 2020 Peter Mjemu akiwa ameshika fomu ya kuwania nafasi ya Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania 
Na Asha Mwakyonde, Dodoma

ALIYEKUWA mgombea nafasi ya Ubunge Jimbo la Chato mwaka 2020 Peter Mjemu amewania nafasi ya Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania akiamini kuwa matatizo ya Watanzania yanatatuliwa ndani ya Bunge.

Akizungumza jijini Dodoma jana na waandishi wa habari mara baada ya kuchukua fomu ya kuwania nafasi hiyo alisema kuwa Bunge la Tanzania ndio kitovu cha maendeleo ya Watanzania na Taifa kwa ujumla katika nchi.

Mjemu ambaye ni mtumishi wa serikali amesema ameamua kuchukua fomu hiyo kwa kuwa anaamini anafaa kushika nafasi hiyo ya juu.

"Taifa bado tunahitaji kujikwamua kiuchumi, bado tunahitaji maendeleo kuna changamoto mbalimbali ambazo zinawakabili vijana kama Taifa na watu kwa ujumla," alisema.

Aliongeza kuwa ameamua kuchukua fomu hiyo ili akasaidiane na wabunge kuliongoza Bunge kwani uwezo ana na kwamba amemaliza degree ya kwanza na ya pili kutoka vyuo vikuu vya Mzumbe na Chuo kikuu cha (UDOM).

Mjemu alieleza kuwa elimu yake inatosha kwenda kuliongoza Bunge na kwamba bado baraka za Mungu zinahitajika.


Post a Comment

0 Comments

KIGOMA YAPATA MWAROBAINI WA UKATILI WA KIJINSIA