Kada wa Chama cha Mapindizi (CCM),Hatibu Mgeja (kushoto), akikabidhiwa fomu ya kugombea nafasi ya Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Mkuu wa Kitengo Cha Uchaguzi wa Chama Cha Mapindizi (CCM), Cuthbert Midala.
Na Asha Mwakyonde, Dodoma
KADA wa Chama cha Mapindizi (CCM),Hatibu Mgeja ametia nia ya kugombea nafasi ya Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo iliachwa wazi na aliyekuwa Spika wa Bunge hilo, ambaye pia ni mbunge wa Kongwa Job Ndugai baada ya kujiuzulu nafasi hiyo.
Akizungumza jijini Dodoma leo Januari 14,2022 baada ya kuchukua fomu hiyo Mgeja amesema kuwa anatimiza haki yake ya kikatiba ya Chama na ile ya Tanzania ambayo inampa mtu haki, mwanachama na mtanzania mwenye sifa ya kugombea nafasi hiyo.
Mgeja amesema lengo la kugombea nafasi hiyo ni baada ya kuguswa na kuona anamchango ndani ya Chama hicho kwa kuwa amelelewa na CCM.
" Nimepata msukumo wa kuja kuchukua fomu ya kuwania nafasi hii baada ya kupata elimu niliyoisoma katika chuo kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM),masuala ya Siasa, Uongozi na Mahusiano ya Kimataifa. Pia nimepta bahati ya kusoma nchini Norway Shahada ya pili ni kwa sababu ya Chama Cha Mapindizi," amesema.
Amesema kama kijana ameona mengi na anatamani kwenda kufanya mabadiliko katika Bunge hilo kwa kuwa uwezo na nia ya kulingoza anayo.
Mgeja ameongeza kuwa endapo atapata nafasi hiyo ataenda mabadilo yatakayo leta taswira mpya katika Bunge hilo.
"Yapo Mambo kama nchi kama Taifa tukiangalia ambavyo Chama Cha CCM chini ya mama yetu Rais Samia kazi na utekelezaji wake umekuwa wa kasi," amesema Mgeja.
Mgeja amesema Serikali inahitaji kuwa na Bunge ambalo litamsaidia Rais kwa ajili ya kutekeleza ambacho amekusudia kutimiza malengo yake yatakayo leta jita kwa Taifa.
0 Comments