Kada wa Chama Cha Mapindizi(CCM),Wilaya Mkinga Mkoani Tanga Hamisi Rajabu (kushoto), akikabidhiwa fomu ya kugombea nafasi ya Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, (Kulia), na Katibu Msaidizi Mkuu Idara ya Oganizetion CCM Taifa Solomon Itunda
Na Asha Mwakyonde, Dodoma
KADA wa Chama Cha Mapindizi(CCM),Wilaya Mkinga Mkoani Tanga Hamisi Rajabu leo amechukua fomu ya kuwania nafasi ya Spika ambayo hivi karibuni aliyekuwa Spika Job Ndugai na nafasi hiyo kuachwa wazi.
Rajabu ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM Wilaya hiyo na Mjumbe wa kamati ya utekelezaji Baraza la Umoja wa Vijana (UVCCM), Mkoa wa Tanga.
Akizungumza na waandishi wa habari Januari 12 ,2022, jijini Dodoma muda mfupi baada ya kutoka kuchukua fomu ya kugombea uspika amesema tangu Bunge lianzishwe mwaka 1956 halijawahi kuongozwa na kijana.
Mbombea huyo ameeleza kuwa lengo kubwa la kuchukua fomu hiyo ya kugombea ni kuhakikisha anarudisha heahima ya Bunge kwenye dira ya kibunge na kufuata sheria zenye kuhakikisha mhimili wa Bunge unafanya kazi kwa ukamilifu.
Amesema kuwa ana haki ya kuwa spika na kuonesha Umma kuwa vijana wanaweza kuongoza Bunge hilo.
Rajabu ameeleza kuwa ni wakati wa vijana kushika nafasi za juu katika uongozi ambayo ni za kufanya maauzi kwani imezoeleka Bunge kuongozwa na wazee.
Mgombea huyo amesema kuwa endapo atapata nafasi hiyo atahakikisha Bunge analisimamia ipasavyo na kwamba wananchi wataona kuwa wamepata Spika sahihi.
Amesema wakati wa mijadala na kuchangia kiti cha Spika kitaelekeza bunge kazi za wabunge,Naibu Mawaziri na Mawaziri na namna ya kuikosoa serikali na kuishauri serikali.
Aidha amesema kuwa katika uongozi wake wa kuliongoza Bunge hatahakikisha kila jambo ndani ya Bunge sheria,Kanuni na misingi yote inaendelea kwa kufuatia misingi.
"Kuna baadhi ya mikataba ambayo inaingizwa ndani ya Bunge ambayo inaingia kwa hati ya dharura na kutokana na hiyo inatakiwa kuangaliwa vizuri hivyo nitahakikisha mambo yanakaa sawa na wananchi hawatajutia bunge hilo kuongozwa na kijana," ameeleza.
0 Comments