Vigogo 30 wa CCM wajitokeza kuwania nafasi ya Spika



 

Katibu Msaidizi Mkuu Idara ya Oganizetion CCM Taifa Solomon Itunda akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Halmashauri ya Taifa (NEC), CCM Shaka Hamdu Shaka.

Na Asha Mwakyonde,Dodoma

WANACHAMA wa chama chama Mapinduzi (CCM),waliochukua fomu za kuwania nafasi ya Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania wafikia 30.

Chama hicho kilifungua pazia la kupokea maombi ya kugombea nafasi hiyo Januari 10 hadi 15 ambayo iliachwa wazi na aliyekuwa spika wa Bunge hilo ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Kongwa Job Ndugai aliyejiuzulu hivi karibuni.

Akizungumza jijini Dodoma Januari 12, 2022, Katibu Msaidizi Mkuu Idara ya Oganizetion CCM Taifa, Solomon Itunda kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Halmashauri kuu ya Taifa (NEC),CCM Itikadi na Uenezi  Shaka Hamdu Shaka amesema wagombea saba wamechukua  katika ofisi ya makao makuu ya chama hicho.

Amesema idadi hiyo inafikia wagombea 30 tangu walipoanza kupokea maombi hayo ambapo wanawake waliojitokeza ni wanne na wanaume ni 26 na kwamba baadhi yao sio wabunge wa Bunge hilo.

Amesema kuwa fomu hizo zinatolewa katika ofisi tatu ambao ni makao makuu ya chama hicho jijini Dodoma, ofisi ndogo ya Lumumba iliyopo jijini Dar es Salaam na iliyopo Zanzibar.

Itunda amewataja wagombe hao kuwa ni mbunge wa Geita vijijini Joseph Msukuma, aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Sophia Simba, aliyekuwa mbunge wa Shinyanga Mjini Stephen Masele, Patrick Nkandi na Hamidu Chamani, 

Katibu huyo amesema kuwa wengine, Juma Chum, Festo John,Gudluck Medee,Baraka Byabato,George Nangale, Zahoro Hanuna, wakili na mwanadiplomasia Barua Mwakilanga, aliyekuwa mbunge wa Bariadi Magharibi Andrew Change,Thomas Kirumbuyo na Angeliana John.

Ameongeza kuwa waliojitokeza katika ofisi ya makao makuu jijini Dodoma ni Dk.Simon Ngatunga, aliyewahi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, ofisa vijana Mwandamizi Mkoa wa Dodoma Tumsifu Mwasamale, aliyekuwa ofisa Tawala wa Mwandamizi wa Wizara ya fedha Idara ya Mhasibu mkuu wa serikali Markion Ndofi  na mbunge wa Mlimba Godwin Kunambi.

Wengine ni Naibu Spika wa Bunge Dk. Tulia Ackson,Ambwene Kajula, mbunge wa Ilala Mussa Zungu, mbunge wa Tabora mjini Emmanuel Mwakasaka, Profesa Handley Mafwenga, Dk.Mussa Ngonyani, mjumbe wa halmashauri kuu CCM Tanga Hamisi Rajabu,  Asia Abdallah na  aliyewahi kuwa wa Maendeleo ya Mifugo Dk. Titus Kamani.

Katibu huyo amaeleza kuwa katika ofisi ya Zanzibar aliyecukua fomu ni  Mhandisi Abdulaziz Jaad Hussein.

Post a Comment

0 Comments

MATIVILA AAGIZA MKANDARASI KUFANYA KAZI USIKU NA MCHANA