Bunge lampitisha Dk.Tulia kuwa Spika

Na Asha Mwakyonde,Dodoma WABUNGE wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania wamempitisha Dk.Tulia Ackson kuwa Spika wa Bunge hilo baada ya mchakato wa kupika kura kumalizika. Dk. Tulia ni mmoja katika ya wagombea 9 wa nafasi hiyo ambapo wapinzani wake hawakupata hata kura moja. Akisoma matokeo hayo jijini Dodoma leo ndani ya Bunge hilo kwa Mamlaka aliyopewa kuwa Mwenyekiti wa muda wa mchakato huo wa uchaguzi aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba,Maendeleo ya Makazi William Lukuvu amesema wabunge walipiga kura ni 376. Akitangaza matokeo hayo Mwenyekiti huyo amesema Dk. Tulia ameshinda kwa kura zote 376 na kumtangaza kuwa Spika wa Bunge hilo. "Kwa Mamlaka mliyonipa namtangaza Dk.Tulia Ackson kuwa Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania," amesema Lukuvu. Wagombea wengine katika nafasi hiyo hawakuambulia kupata kura hata moja na pia Dk.Tulia ni Spika wa pili kwa mwanamke baada ya mtangulizi wake Anne Makinda. Kwa upande wake Dk.Tulia amewashukuru wabunge waliompigia kura na kuahidi kushikamana nao katika kuhakikisha wanawaletea wananchi Maendeleo. " Natoa shukurani zangu za dhati kwa chama changu kuweza kuniamini na kunipisha na kuniona nafaa katika nafasi hii," amesema Dk. Tulia. Ameongeza kuwa asingefika katika nafasi hiyo kama sio wabunge wa chama chake kumpigia kura.

Post a Comment

0 Comments

KIGOMA YAPATA MWAROBAINI WA UKATILI WA KIJINSIA