Ewura:Kuna uwezekano wa mafuta kupanda bei Machi na Aprili

Kaimu Mkurugenzi Mkuu kutoka Mamlaka ya Udhibiti Wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA),Mhandisi Godfrey Chibulunje akizungumza na waandishi wa habari hawapo (pichani) wakati akitoa mwenendo wa bei za mafuta nchini. Na Jasmine Shamwepu,Dodoma. KAIMU Mkurugenzi Mkuu kutoka Mamlaka ya Udhibiti Wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Godfrey Chibulunje amesema kuna uwezekano mkubwa wa kuongezeka kwa bei za mafuta  kwa mwezi Machi na Aprili 2022.  Hayo ameyasema leo jijini hapa na Kaimu Mkurugenzi huyo wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo wakati akitoa taarifa ya kuhusu mwenendo  wa bei za mafuta  nchini. Amesema katika kufuatilia mwenendo wa bei za mafuta katika soko la dunia mafuta yanaweza kupanda ifikapo Mwezi  Machi na Aprili.  " Kutokana na hayo EWURA  itaendelea kufutailia mwenendo  huo kwa karibu ili kuishauri serikali hatua za kuchukua katika harakati za kupunguza makali ya bei za mafuta," amesema  Chibulunje.  Hata hivyo akieleza bei za mafuta kwa Mwezi Februari amesema bei za rejareja za mafuta ya petroli, dezeli  na mafuta ya taa yaliopelekwa bandari ya Dar es Salaam  zimepungua kwa shilingi 21 kwa lita  ya mafuta ya Petroli na shilingi 44 kwa lita ya mafuta ya taa, huku bei ya mafuta ya Dezeli  ikiongezeka kwa shilingi  13 kwa lita. Aidha ameeleza kwamba bei  rejea kwa mafuta ya petroli  na dezeli kwa mikoa ya Kaskazini  Tanga, Kilimanjaro Arusha na Manyara zimepungua kwa shilingi  123 kwa lita ya petroli na shilingi 92 kwa dezeli. "Bei za rejea za mafuta petroli na dezeli kwa Mikoa ya kusini Mtwara Lindi na Ruvuma zitaendelea kuwa zile zile zilizotangazwa katika toleo la tarehe 5 Januari 2022," Amesema Chibulunje.

Post a Comment

0 Comments

KIGOMA YAPATA MWAROBAINI WA UKATILI WA KIJINSIA