Haya ndio madhara ya kujifungua kwa njia ya upasuaji

Daktari Bingwa wa Magonjwa ya akina mama na Uzazi kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili (MHH), Dkt. Living Colman akizungumzia madhara ya kufanyiwa upasuaji. Na Asha Mwakyonde, Dar es Salaam KUTOKANA na ongezeko la Sayansi na Teknolojia ya mitandao ya kijamii akina mama wamekuwa wakiingia You Tube na kuangalia namna mama anavyojifungua. Kuumwa uchungu ni kazi ngumu ndio maana ikatwa leba hivyo akina mama wakiangalia hasa wadada wenye ujauzito wa kwanza wakiangalia wanaogopa kupitia maumivu aliyaona kupitia midandao ya kimaii. Kuna kuongeza njia, mtoto anaweza akavutwa hivyo huingiwa na hofu na kuchangua njia rahisi ya kufanyiwa upasuaji kwani muda wa kuumwa uchungu unaweza kuchukua saa 10 wakati kufanyiwa upasuaji ni nusu saa au saa moja. Kutokana na njia hizo ndio maana wadada wengi wanachagua upasuaji wanahisi haitakuwa na mateso kwao. Kujifungua kwa upasuaji ni njia mojawapo ya akina mama kujifungua inayoweza kutumika kuokoa maisha ya mama na mtoto. Njia hii inahusisha kupewa dawa ya usingizi anaweza kupewa general maana ya jumla nusu kaputi kitaalimu General Anesthesia au akapewa nganzi ya mgongoni Spinal Anesthesia. Katika njia hizi mbili inayoonekana ni salama ni njia ya ganzi mgongoni zamani walikuwa wakitumia zaidi njia ya nusu kaputi lakini ikaonekana kama ina madhara kwa mama na mtoto kwa sababu inahusisha utaalamu zaidi. Dawa za usingizi zinaweza zikapenya moja kwa moja kwenye kondo la mtoto kabla hajatolewa akavuta dawa hizo. Baada ya Sayansi kuendelea ikaonekana kuna njia ya ganzi ambayo mama anachomwa mgongoni halafu anapewa dawa ambayo inamuwekea ganzi kati ya usawa wa kitovu na kushuka chini maana anafanyiwa upasuaji akiwa anajitambua. Ikaonekana njia hiyo ni salama kidogo kwa mama na mtoto kwa maana haimzuru na haiingii kwa mtoto huyo. MADHARA YA UPASUAJI Akizungumzia madhara ya upasuaji Daktari Bingwa wa Magonjwa ya akina mama na Uzazi kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili (MHH), Dkt. Living Colman anasema maumivu ya migongo hayo ni madhara tarajiwa (Side effects), mgonjwa anaweza kuyapata baada ya kufanyiwa upasuaji kutokana na sababu mbalimbali. Daktari huyo anasema sindano ile ya mgongoni wakati mama anawekewa inaweza ikagusa mshipa wa fahamu na kwamba kuna aina fulani ya sindano hiyo ni nene kidogo hivyo wakati inapenya inaweza ikaweka kovu. Anafafanua kuwa kuna madhara ya haraka yanaweza kutokea baada ya upasuaji au ambayo ni ya muda mrefu. "Wakati sindano inachomwa Kuna ute ute ambao upo kwenye mgongo unaotoka endapo utatoka kwa wingi kidogo inaweza kusababisha mama akapata maumivu ya kichwa baada ya zile siku mbili au tatu za upasuaji," anasema. Dkt. Colman anaongeza kuwa hali kama kizungu zungu pamoja na maumivu ya migongo kwa wakati huo. Anaeleza kuwa kuwa kuna madhara ya muda mrefu ambayo yanaweza yakakaa miaka kadhaa ni pamoja na lile kovu ama mshipa wa fahamu ambao umeguswa inawezekana ukawa umepata ufa. Pia daktari huyo anasema wakati wa baridi hali ya kawaida mama anaweza kulalamika maumivu ya migongo ya hapa na pale. TIBA Dkt. Colman anabainisha kuwa tiba yake ni pamoja na kufanya mazoezi, kupewa dawa za maumivu. WITO KWA AKINA MAMA Daktari huyo anasema njia za kujifungua zipo za aina mbili kujifungua kwa upasuaji na kwa njia ya kawaida. Anasema kujifungua kwa kawaida ndio njia sahihi ambayy ni salama kama kila kitu kikienda vizuri kwa sababu kurudia katika hali ya kawaida kunachukua kuda wa saa 24 hadi 48 au ndani ya siku saba ama nane tofauti na njia ya upasuaji ambayo inachukua muda kidogo. " Katika hizi njia lazima kutakuwa na sababu kwa nini mtu anafanyiwa upasuaji zinaweza kuwa ni kwa mtoto au kwa mama lengo ni kuokoa maisha ya mama na mtoto," anaeleza Dkt. Colman. Anafafanua sababu za mtoto mama anaweza akawa abaumwa uchungu na mtoto huyo anapata shida ya mapigo ya moyo yanaenda vibaya inabidi afanyiwe upasuaji ama kila kitu kipo vizuri lakini njia haifunguki. "Kuna upasuaji mwingine labda mimba ya kwanza na hakuna sababu ya kitaalimu siyo ya mtoto wala ya mama lakini anaomba," anasema Dkt. Colman. Anasema kwa maadili ya kidaktari mgonjwa anahaki ya kuchagua njia ya tiba na anapo omba wanajaribu kimweleza madhara ambayo anaweza kuyapata yakiwamo maumivu ya mgongo. Daktari hiyo anaeleza kuwa kama mgonjwa anasisitiza anataka njia hiyo ya upasuaji kwa kuwa ni haki yake wanamfanyia. USHAURI " Wamuachie mtalaam aamue kama kuna sahabu maalumu mtu kufanyiwa upasuaji ikiwa hivyo madhara hayatatokea na kila kitu kitakuwa salama kwa sahabu kila upasuaji lazima kuna sababu," anasema. Anasema katika madhara yanayotokana na upasuaji ni pamoja na maumivu ya mgongo na kichwa. Dkt. Colman anasema kuna vitu ambavyo wanavishauri kwa mgonjwa ndani ya muda wa saa 24 ili kupunguza maumivu hayo. " Anatakiwa awe katika hali ya utulivu akiwa amelala kitandani bila kunyanyua kichwa kwa muda wa saa 8 hadi 12, " anaeleza. Dkt. Colman anasema mgonjwa wa upasuaji anapoaanza kunywa chai na maji anashauriwa anywe maji mengi kidogo na kutokuongea mara kwa mara katika kipindi hicho. Anasema inaweza kupunguza kidogo maumivu hasa ya kichwa.

Post a Comment

0 Comments

KIGOMA YAPATA MWAROBAINI WA UKATILI WA KIJINSIA