WANYAMA PORI WANAVYOONGEZA PATO LA NCHI


Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Damas Ndumbaro akizungumza na waandishi wa habari wakati akizungumzia mafanikio ya mwaka mmoja wa Rais Samia Suluhu Hassan.

Na Asha Mwakyonde,Dodoma

ZAIDI ya asilimia 80 ya Utalii wa Tanzania unategemea wanyama pori hii inatokana na jitihada zinazofwa na Wizara ya MaliAsili na Utalii za kuliimarisha Jeshi la Uhifadhi wanyama pori na Misitu.

Utalii wa wanyama Pori umekuwa ukiliongezea Taifa mapato yatokanayo na watalii wa kimataifa yanadiriwa kuongezeka kutoka Dola za kimarekani milioni 714.59 mwaka 2020 hadi Dola milioni 1,254.4 mwaka 2021 sawa na ongezeko la asilimia 76.

Licha ya kuwapo kwa janga la ugonjwa UVIKO-19, sekta ya utalii imeweza kuongeza idadi ya watalii wa nje katika kipindi cha ungonjwa huo kutoka watalii 620,867 mwaka hadi kufikia 922,692 mwaka 2021 sawa na ongezeko la asilimia 48.6.

Dk. Damas Ndumbaro ni Waziri wa Maliasili na Utalii ameeleza kuwa mafanikio ya mwaka mmoja wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema ufanisi huo umetokana na mikakati mbalimbali inayochuliwa na  serikali kurejesha sekta ya utalii katika hali yake.

Amesema pamoja na mlipuko wa jana la UVIKO-19 ambapo limeathiri kwa kiasi kikubwa sekta ya utalii nchini Taifa limeendelea kuwa stamilivu  katika kukabiliana na jana hilo.

Dk. Ndumbaro ameeleza kuwa idadi ya watalii wa kimataifa katika kipindi cha mwaka 2021 na kwamba idadi ya watalii wa ndani waliotembelea maeneo ya hifadhi imeongezeka kutoka 562,549 mwaka 2020 hadi watalii 788,933 mwaka 2021 sawa na ongezeko la  asilimia 40.2.

" Mapato yatokanayo na Utalii wa ndani katika maeneo yaliyohifadhiwa yaliongezeka kutoka shilingi bilioni 9.7, mwaka 2020 hadi kufikia  bilioni  12.4, mwaka 2021, sawa na ongezeko la asilimia 27.8," amesema Dk. Ndumbaro.

UVIKO-19

Amesema katika utekelezaji wa mpango wa mapambano dhidi ya ugonjwa wa UVIKO-19,serikali  aendelea na kutekeleza mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa dhidi ya ugonjwa huo ambapo Wizara hiyo imetengewa kiasi cha shilingi bilioni 90.2 sawa na asilimia 6.9 ya fedha yote kwa ajili ya shughuli za mbalimbali za miradi.

" Fedha hizi zitatumika katika kuboresha Utendaji wa sekta ikiwa ni pamoja na kuziwezesha taasisi za Wizara zilizoathirika kutokana na mlipuko wa UVIKO-19, kuimarisha masoko na Utangazaji Utalii, mazingira ya biashara ya utalii kwa kuzingatia viwango vya afya na usalama vya kitaifa na kimataifa," amesema.

Pia Dk.Ndumbaro ameongeza kuwa fedha hizo zitatumika katika kuboresha miundombinu kwenye maeneo ya vivutio vya Utalii wa nchi, Kutoa mafunzo kwa watoa huduma za Utalii kuhusu namna ya kuendesha biashara za Utalii hususani wakati wa majanga mbalimbali  yanayotokea nchini.

MISITU

Pia ameeleza kuwa Wizara hiyo imeendelea kuongeza jitihada za kuimarisha Ulinzi na Uhifadhi wa rasilimali za Maliasili ambazo zinatumika kwa njia endelevu kwa manufaa ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.

Aidha amesema katika kipindi cha mwaka mmoja wa Rais Samia Wizara hiyo imepata mafanikio mengi ndani na nje ya nchi ikiwamo kupata tuzo mbalimbali ya utalii bara ( Continental Tourism Award ya mwaka 2021), iliyotolewa na Bodi ya Utalii ya Afrika ( African Tourism Board), wakati wa onyesho la kwanza la EARTE iliyofanyika jijini Arusha mwaka jana.

Kwa upande wake Debora John ambaye ni mwananchi aliyetembelea Hifadhi ya Ruaha ambayo ipo katikati ya Tanzania katika umbali wa kilometa 131 magharibi kwa mji wa Iringa.

Hifadhi ya Taifa ya Ruaha ambayo ina ukubwa wa zaidi ya kilomita mraba 20,000 za ardhi, ni mbuga ya pili kwa ukubwa Tanzania baada ya Hifadhi ya Taifa ya Nyerere (Selous).

Ameeleza kuwa kuna faida nyingi za kutembelea Hifadhi na Maliaasili zikiwamo kuchangia ukuaji wa uchumi wa nchi kwa kuongeza mapato ya ndani pamoja na kupata marafiki mbalimbli ndani na nje.

 








Post a Comment

0 Comments

WAUGUZI, WAKUNGA ENDELENI KUBEBA DHAMANA KAMA SERIKALI ILIVYOWEKEZA