MAKINDA:SENSA YA MWAKA HUU HAKUNA ATAKAYEACHWA INAFANYIKA KIDIGITALI


Kamisaa Sensa ya Watu na Makazi Tanzania Bara Anne Makinda

Na Asha Mwakyonde,Dodoma

VIONGOZI,Watendaji wa Mitaa wametakiwa kuwa wazalendo katika zoezi la Utengaji wa maeneo ya Kuhesabiwa Watu kwa ajali ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022, kutokana na serikali kutokuwa na fedha za kutosha.

Pia Watendaji wametakiwa kutoa ushirikiano kwa viongozi watakao husika na zoezi la utambuaji wa mipaka katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dodoma ambalo linatarajiwa kuanza leo.

Hayo yamesemwa Machi,22, 2022 jijini hapa na Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi Tanzania Bara  Anne Makinda, katika mkutano wa Maandalizi ya zoezi la Utengaji wa maeneo ya Kuhesabiwa Watu kwa ajali ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022, amesema viongozi hao wanajua sensa ya mwaka huu serikali haina fedha za kutosha lakini kunahiji uzalendo.

Makinda ameeleza kuwa sensa ya mwaka huu inafanyika kitaalamu na kwamba hakuna mtu atakayeachwa katika zoezi la kuhesabiwa pindi litakapofika Agosti mwaka huu.
Amesema zoezi la kuhesabu linafanyika katika mitaa ambayo imepangiliwa kwa uhakika na kwamba wanataka  sensa hiyo itakayofanyika ipate sifa ndani  na nje ya nchi.

Makinda ameongeza kuwa Wenyeviti wa mitaa wanawajua watu wote wa mitaani kwao  kwa majina hivyo kwa serikali ni watu muhimu kuliko wote.

Amesema faida ya  sensa ni serikali kutaka kujua aina ya makundi, idadi ya watu ili iweze kuandaa  bajeti na kwamba katika sensa hiyo wataandaa mafunzo ya siku 21 kwa makarahani watakaohusika kuhesabu sensa hiyo.

"Katika sensa hii tutatoa mafunzo, semina  ya siku 21 kwa vijana ambao hawana kazi na watafanya mitihani na atakaye feli basi hatahusika katika zoezi hili," amesema Makinda.

Naye Kamisaa wa Tanzania Visiwani  Balozi Hamza Mohamed amesema katika sensa kuna mambo mengi na kila jambo linatakiwa kupewa uzito wake.

Amesema Tanzania mpya ambayo itakuwa na maendeleo makubwa ya kiuchumi inategemea taarifa ambazo zitakusanywa kupitia Sensa ya Watu na Makazi.

Kwa upande wake Mratibu wa Sensa Taifa Seif Kuchengo amesisitiza juu ya suala la kutaka ushirikiano kwa Watendaji hao.

Awali Kaimu Kaimu Mtakwimu Mkuu wa Serikali Ruth Minja amesema kuwa maandalizi ya zoezi hilo yamekamilika kwa asilimia 70.

Minja ameeleza kuwa tayari wameshaandaa nyezo zote za kazi na  sensa ya mwaka huu inaenda kufanyika kidigitali ifikapo Agosti mwaka huu.




Post a Comment

0 Comments

WAUGUZI, WAKUNGA ENDELENI KUBEBA DHAMANA KAMA SERIKALI ILIVYOWEKEZA