LAMBERT ALIPUKA BUNGENI AWATAJA ROMA NA AZORY


 Mbunge wa Viti maalum Chadema Agnesta Lambert akichangia bajeti ya Wizara ya  Katiba na Sheria iliyowasilishwa bungeni.

Na Mwandishi wetu, Dodoma


MBUNGE wa Viti Maalumu wa chama Cha Demokrasia na Maendeleo ( CHADEMA),Agnesta Lambert amesema Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB),ni mfu kwa kuwa imekuwa kimya hata yakitokea matukio mbalimbali ya uvunjifu wa haki hapa nchini.

Aidha Lambert alisema licha ya kuwa tume hiyo imekuwa kimya lakini hata Serikali imeshindwa kuwapa fedha katika bajeti za Wizara husika jambo ambalo linalochangia kuzorota kwa utendaji wa tume hiyo.

Lambert aliongea hayo jana Bungeni Jijini hapa alipokuwa akichangia mchango wa Bajeti ya Wizara ya Sheria na Katiba iliyowasilishwa jana Bungeni hapo.

‘’Mimi nashangaa hii tume imekuwa mfu kabisa, yametokea matukio mengi ya kuvunja haki za binadamu hapa nchini lakini hatujawai kusikia tume hiyo ikitoa tamko hata la kulaani tu’’, alisema.

Aidha Lambert alitolea mfano matukio ya kutekwa kwa baadhi ya watu mfano Roma mkatoliki, Azory ambaye mpaka leo hajapatikana na hajulikani alipo hata matukio yaliyotokea hivi karibuni mtwara Polis kuua wananchi hakuna tamko lolote.

‘’Yaani hii tume ndio maana nasema ni mfu, juzi juzi hapa yametokea muaji huko Mtwara Polis kaua mwananchi, mpaka Rais Samia katoa tamko la kulaani mauaji hayo, lakini tume hiyo iko kimya, sasa inafanya kazi gani?

Mbunge huyo machachari kijana alisema kuwa hata Serikali imeshindwa kutoa pesa kwenye bajeti kuwapa ili waweze kutekeleza majukumu yao.

Aidha Lambert alisema katika bajeti ya mwaka 2021/2022 tume hiyo ilipata Sh. 373 kutoka nje  wafadhili  lakini Serikali haijatoa fedha, na bajeti ya 2022/2023 Tume hiyo inapatiwa Sh. Millioni 260  huku Serikali ikishindwa kuwapa fedha.

Mbunge huyo alisema kitendo cha Tume hiyo kutegemea fedha kutoka kwa wafadhili tu, kinawanyima haki na kukosa wigo mpana wa kutekeleza majukumu yao kwani fedha wanazopewa na wafadhili ni ndogo hazitoshi.

‘’Tume  hiyo ina haki ya kutembea katika maeneo mbalimbali kama vile magerezani, mashuleni kuangalia utendaji wa haki za binadamu unavyofanya kazi, lakini hicho kitu hakuna wala hatujawahi kusikia’’, alisema Lambert.

Mbunge huyo alisema ili tume hiyo iweze kuwa imara Serikali inatakiwa kuwapa fedha tume hiyo kwani  za wafadhili pekee haziwezi kutimiza majukumu yake kikamilifu hapa nchini.


Post a Comment

0 Comments

DKT. BITEKO ASISITIZA UMUHIMU WA MIFUMO THABITI YA NISHATI JADIDIFU KUKIDHI MAHITAJI YA NISHATI