VIONGOZI WA VYAMA VYA WAFANYAKAZI NCHINI WAJENGEWA UELEWA KUSIMAMIA MIFUMO SERIKALINI

 


Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Jenista Mhagama,akizungumza wakati wa kikao kazi kati ya serikali na viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi nchini chenye lengo la kuwafahamisha  kuhusun mifumo mbalimbali serikalini iliyojengwa ili kuboresha utumishi wa umma leo April 9,2022 jijini Dpodoma.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu),Joyce Ndalichako ,akizungumza kwenye kikao kazi kati ya serikali na viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi nchini  leo April 9,2022 jijini Dpodoma.

Naibu Katibu Mkuu,Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bw.Xavier Daudi,akielezea lengo la kikao kazi kati ya serikali na viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi nchini  leo April 9,2022 jijini Dpodoma.


Baadhi  ya washiriki wakifatilia mada mbalimbali  wakati wa kikao kazi kati ya serikali na viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi nchini chenye lengo la kuwafahamisha  kuhusun mifumo mbalimbali serikalini iliyojengwa ili kuboresha utumishi wa umma leo April 9,2022 jijini Dpodoma.

Na Asha Mwakyonde,Dodoma

WAZIRI wa Nchi,Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Jenista Mhagama amesema kuwa wanapofanya maboresho ndani ya serikali lengo lao ni kuimarisha vyama vya wafanyakazi kwani  wanahitaji msaada mkubwa kutoka kwa watumishi wa Umma vinginevyo hawatafika wanapotaka.

Pia Waziri Mhagama  amesema ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wameamua kupokea na kuzingatia maono ya Rais Samia Suluhu Hassan ya muda mfupi na mrefu.

Hayo ameyasema jijini hapa Aprili 9, 2022 wakati akizungumza na viongozi wa vyama vya wafanyakazi nchini  kwa lengo la kuwahamasisha mifumo mbalimbali serikalini iliyojengwa ili kuboresha Utumishi wa Umma  katika  kikao kazi cha kuwajengea uelewa viongozi hao namna ya kutekeleza majukumu yao amesema serikali imekuwa ikifanya mabadiliko mengi yakiwamo ya kimfumo.

Waziri huyo ameeleza kuwa  hatua hiyo ya kuwajengea uelewa  itawawezesha kwenda kuwaelimisha watumishi wa umma katika utekelezaji wa majukumu yao bila shuruti.
                                  
Waziri Mhagama ametaja mifumo iliyojengwa katika ofisi yake kuwa ni pamoja na  Mfumo mpya wa Usimamizi wa Utendaji Kazi kwa Watumishi wa Umma (PEPMIS) uliolenga kuondoa changamoto za usimamizi wa utendaji kazi zilizojitokeza katika utekelezaji wa mfumo wa awali wa OPRAS, ambao haukuakisi hali halisi ya utendajikazi wa watumishi wa umma.

“Mfumo mpya wa PEPMIS utakuwa ni wa kielektroniki na utaondokana na matumizi ya makaratasi,pia utaongeza uwazi katika usimamizi wa watumishi na kuondoa upendeleo na uonevu katika upimaji wa utendaji wa watumishi..,pia mfumo huu pia utahamasisha uwajibikaji wa hiari na kurahisisha upatikanaji wa taarifa za utendaji kazi wa watumishi.”

Aidha ameutaja mfumo mwingine kuwa ni Mfumo mpya wa Usimamizi wa Utendaji kazi katika ngazi ya Taasisi (PIPMIS) mfumo ambao amesema ni makubaliano ya kimaandishi kati ya Serikali na Taasisi ya Umma kuhusu malengo ambayo Taasisi husika itayatekeleza katika kipindi cha mwaka mmoja huku akisema mfumo wa huo wa PIPMIS utaongeza uwajibikaji katika utekelezaji wa sera, mikakati na vipaumbele vya taasisi, sekta na taifa kwa ujumla.

“Kusimamia rasilmali zote nchini tulizonazo,mipango ya maendeleo,mipango fedha  na mipango mingine,na tukiweza kufanya kazi kwa pamoja ,tukaelewana,tukabainisha changamoto tulizo nazo lakini tukazingatia sheria na taratibu mwisho wa siku tutakuwa tumetoa mchango mkubwa sana katika maendeleo na ustawi wa Taifa letu.”amesema Mhagama.

Ameongeza kuwa  tayari  Rais ametoa kibali cha kuajiri watumishi 32,000 ,hivyo  vyama vya wafanyakazi watakuwa wameula kwa kuwa  atakuwa amejenga nguvu ya kutosha kwa wafanyakazi kwa kuongeza idadi ya wafanyakazi hao  mambo mengine kupitia wananchama yataongezeka na kuimarika.
                                             
Ametaja mifumo iliyojengwa katika ofisi yake kuwa ni pamoja na  Mfumo mpya wa Usimamizi wa Utendaji Kazi kwa Watumishi wa Umma (PEPMIS) uliolenga kuondoa changamoto za usimamizi wa utendaji kazi zilizojitokeza katika utekelezaji wa mfumo wa awali wa OPRAS, ambao haukuakisi hali halisi ya utendajikazi wa watumishi wa umma.

“Mfumo mpya wa PEPMIS utakuwa ni wa kielektroniki na utaondokana na matumizi ya makaratasi,pia utaongeza uwazi katika usimamizi wa watumishi na kuondoa upendeleo na uonevu katika upimaji wa utendaji wa watumishi..,pia mfumo huu pia utahamasisha uwajibikaji wa hiari na kurahisisha upatikanaji wa taarifa za utendaji kazi wa watumishi.”

Amesema,Ofisi ya Rais Menejementi ya Utumishi wa Umma imeendelea kuimarisha utekelezaji wa Sera ya Serikali Mtandao na kujenga mifumo ya TEHAMA inayohusu uendeshaji wa Serikali wa kila siku na kurahisisha utoaji wa huduma bora kwa umma.

Mhagama amesema,Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma imefanikiwa kujenga Mfumo wa Sema na Waziri , Mfumo wa e-mrejsho, Mfumo wa Dawati la Huduma kwa Mteja maarufu kama UTUMISHI Call Centre ,Mfumo maalum wa Tathmini ya hali ya Mfumo wa Huduma Mtandao kwa Watumishi (Watumishi Portal).

Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu)  Joyce Ndalichako amebainisha kuwa pamoja na juhudi za serikali za kupima utendaji kazi serikalini  Rais amelekeza ushirikishwaji wa Vyama vya Wafanyakazi ili waendelee  kuwa daraja kati ya waajiri na Wafanyakazi kwa kuchochea na kuhimiza utamaduni kwa Wafanyakazi kudai haki na kutimiza wajibu wao.

Ameongeza kuwa Ofisi ya Waziri Mkuu- Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu imeendelea kutekeleza maagizo ya  Rais kwa kukamilisha Mfumo wa Kielektroniki wa utoaji wa Vibali vya Kazi kwa raia wa kigeni ambao  umepunguza muda wa kushughulikia maombi ya vibali vya kazi kutoka siku za kazi 14 hadi siku 7.

Naye Rais wa shirikisho la wafanyakazi nchini TUCTA Tumaini Nyamhokya  amesema,wao kama viongozi wa vyama vya wafanyakazi wanachopenda ni wafanyakazi kuwajibika na kufanya kazi kwa bidii na kwamba kinachotakiwa mifumo isiwe ni ya kunyanyasa wafanyakazi hasa kuwatumikisha zaidi ya muda wa kazi na bila mwajiri kutambua hilo.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Nchini (CWT) Deus Seif  amesema,mfumo wa awali wa OPRAS ulikuwa na changamoto nyingi hasa kwa walimu huku akisema anaamini mfumo unaokuja wa upimaji kazi utaweka mazingira sawa kwenye kupima utendaji kulingana na mazingira ya halisi na hivyo kufanya watumishi wa umma waufurahie utumishi wao.



Post a Comment

0 Comments