WAZIRI NAPE AFANYA ZIARA NCHI NZIMA KUHAMASISHA WANANCHI UMUHIMU WA ANWANI ZA MAKAZI NA POSTI KODI


Waziri  wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa have (have pichani), katika uwanja wa ndege jijini hapa kabla ya kuanza ziara ya kuzunguka nchi nzima kwa lengo la kuhamasisha uwekaji wa Anwani za makazi na pisti kodi.


Na Asha Mwakyonde, Dodoma

WAZIRI wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye amesema kuwa hadi sasa ni asilimia 69 tu ya maeneo yote nchini zoezi la uwekaji wa Anwani za makazi na posti kodi ndio limekamilika.

Nape pia ametaja baadhi ya mikoa ambayo haijafanya vizuri katika zoezi hilo ukiwamo mkoa wa Dar es Salaam huku akitaka zoezi la uwekaji wa Anwani za makazi na posti kodi kukamilika kabla ya Mei 25, ambapo ndio mwisho wa zoezi hilo huku akiwataka wananchi kuhamasika na kuona umuhimu wa mfumo wa Anwani za makazi na posti kodi hizo.

Waziri Nape ameyasema hayo leo Aprili  11,2022  jijini Dodoma wakati akijiandaa kuelekea Mikoa ya Tanga,Kilimanjaro na Arusha kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi kwa lengo la kubaini sababu zinazokwamisha zoezi hilo kutokana na baadhi ya mikoa kutokufanya vizuri na kuhakikisha kila mkoa wananchi wanahamasika na kujua umuhimu wa Mfumo wa Anuani za makazi na post kodi .

Amesema ku Mkoa wa Lindi unafanya vizuri katika zoezi hilo lakini kuna mikoa ikiwemo Dar es Salaam hawafanyi vizuri  huku akiomba kuongezwa kwa jitihada  katika kukamilisha uwekaji wa Anwani za makazi na piati kodi kwani mwezi ujao Mei 25 ndio mwisho.

Pia amewataka wamanchi kutambua kuwa jambo hilo la Anuani ya Makazi na Posti kodi ni la kwao hivyo kila mmoja aone aibu kukaa bila kuwa na anuani za makazi.

"Kila mmoja aone  aibu ni kwa nini hadi  sasa hana anuani ya makazi  jambo hili ni la kwetu sote na ni faida ya kila mmoja wwtu litakusaidia kupata huduma bila kuchelewa," amesisitiza Waziri huyo.

Waziri Nape amefafanua kuwa Ziara hiyo wanatarajia  kupita mikoa mitatu hadi minne kwa siku ili kuendana na muda mchache  ambao umebaki na kwamba kufanya ana imani kila mwananchi atapata hamasi ya kutosha kuhakikisha anaingia kwenye mfumo huo wa anuani za makazi.




Post a Comment

0 Comments

TAWA YAPOKEA TUZO KUTOKA KWA TAASISI YA FOUNDATION FOR DISABILITIES HOPE (FDH)