PROF. MKENDA: MFUMO WA ELIMU UNAHITAJI MABORESHO ILI KULETA MAGEUZI KWA TAIFA


Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda akisisitiza jambo kwa washiriki (hawapo pichani), wakati akigungua mkutano 30 ambao ni wa  siku mbili wa Baraza la wafanyakazi wa wizara hiyo.

Mwenyekiti wa Baraza la wafanyakazi wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Eliamani Sedoyeka alifafanua jambo katika miutano wa 30 wa Baraza hiyo.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Walimu Tanzania (CWT) Deus Seif akitoa neno la shukurani kwa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda ( hayupo pichani),katika mkutano wa 30 wa Baraza la wafanyakazi wa siku mbili wa Wizara hiyo.

Baadhi ya washiriki wa mkutano wa 30 wa Baraza la wafanyakazi wa siku mbili wa Wizara hiyo.

Na Asha Mwakyonde,Dodoma

Waziri wa elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa.Adolf Mkenda amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan wa kuwapatia fedha kwa ajili ya miradi mbalimbali ikiwamo ya ujenzi wa vyuo vinavyoendelea kujengwa nchini ambapo vinatarajiwa kukamilika ifikapo mwisho wa mwezi Juni mwaka huu.

Pia prof. Mkenda amesema kuwa mfumo wa Elimu nchini unahitaji maboresho zaidi ili kuleta maegeuzi kwa taifa na kuhakikisha vijana wanapomaliza shule wawe na uwezo wa kujiajiri au kuajiriwa huku akilitaka Baraza la wafanyakazi walioketi kujadili maendeleo ya wizara, haki za wafanyakazi na maslahi.

Prof.Mkenda ameyasema hayo  leo Aprili 11,2022, Jijini hapa wakati akifungua mkutano wa 30 wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo   wa siku mbili wenye kujadili na kupitisha bajeti ya wizara hiyo ya mwaka 2022/ 2023 kabla ya kupelekwa bungeni ambayo ina kauli mbiu isemayo "Sensa ya Watu na Makazi ni Msingi ni Kichocheo cha  Sera Bora na Mipango  Endelevu ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Tushiriki Kikamilifu, amesema ni vema Baraza hilo likapitia Maandalizi ya bajeti yao ambayo inatarajiwa kusoma Mei 9, mwaka huu.

Amesema kuwa ni wajibu wao kuwashirikisha wafanyakazi hao kwa kuwa wengi wanatoka katika vyuo vya elimu nchini  na kwamba michango yao itasaidia wizara hiyo huku akiwataka  kupitia Mfumo mzima wa Elimu pamoja na Sera zake  ikiwemo Mitaala  ili kuhakikisha taifa linanufaika na wataalamu wanaotokana na Elimu hapa nchini.

Prof. Mkenda ameongeza kuwa  miradi mingi inayoendelea katika wizara hiyo yaliopo mbele yao ikiwamo miradi mbalimbali kwenye vyuo vya elimu, vyou vya  Ufundi Stadi (VETA), na kwamba baadhi ya miradi hiyo wanawajibu wa kukamilisha kwa wakati.

"Elimu ni uwekezaji wa vizazi na vizazi ukiwekeza kwenye elimu leo unawekeza katika nchi yetu kizazi kimoja na kingine na kingine hadi kingine na uwekezaji mzuri kwenye elimu unahakikisha ubora wa elimu wa sasa hadi vizazi vijayo na tukikosea leo huko mbele makosa yatakuwepo," amesema Prof. Mkenda.

Waziri huyo ameeleza kuwa nchi zilizoendelea kielimu tofauti yao ipo katika elimu sayansi na Teknolojia na kwamba nchi zinapishana kwa mapato na kigezo kikubwa sio rasilimali, sio dhahabu, mafuta zipo nchi tajiri zina madini mbalimbali lakini zinapigana vita kila siku.

Amesema miradi yote iliyopo kwenye wizara wataiangalia vizuri na kuangalia ubora wa elimu ambapo hata Rais Samia aliwahi kulizungumzia hilo wakati akiapishwa kuwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Ameeleza kuwa  ubora wa elimu nchini  unapaswa kupitiwa upya ili kumuandaa kijana kuwa mtaalamu na kwamba wanahitaji kuandaa Mtaala uliokamilika kwa sababu elimu haijakamilika haimuandai kijana katika viwango vinavyotakiwa.

Prof. Mkenda amebainisha kuwa kuna haja ya kupitia upya Sera na mfumo wa elimu kwani wana wajibu wa kutoa wataalamu wenye ubora na sio wataalamu wengi wasio na ubora.

Amesema kuwa watashirikiana na Wizara ya Afya kuhakikisha wanapata Madaktari wenye uwezo wa kutosha kwani kumekuwa na namba kubwa ya madaktari lakini bado wagonjwa wanasafiri nje ya nchi kupata matibabu wakati wataalamu wapo hapa nchini.

"Najiuliza sana hawa Madaktari wetu wangepimwa kwa mfumo kamili kabisa wa elimu hii leo tusingekuwa na safari za kwenda nje ya nchi kutafuta matibabu fulani kwani tungeweza kumaliza kila kitu hapa nchini ila naamini tukibadilisha Sera na mifumo yetu naamini tutazalisha wataalamu waliokamilika ili kulisaidia taifa letu"Amesisitiza Prof.Mkenda

Pamoja na hayo Prof.Mkenda amesema kuwa ubora wa elimu unakwenda sambamba na miundombinu bora na salama ya kujifunzia hivyo amewataka watumishi wa wizara hiyo kuhakikisha wanasimamia miradi inayoendelea ikamilike kwa wakati kwa sababu elimu ndio urithi wa vizazi vyote.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza hilo Ambaye pia ni katibu wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Prof.Eliamani Sedoyeka amesema kuwa baraza hilo lipo tayari kuhakikisha taratibu za Wafanyakazi na za uandaaji wa rasimu ya bajeti ya mwaka 2022/2023 ya wizara hiyo unaendelea kujikita katika kuwekeza kwenye maboresho ya elimu lengo likiwa ni kuwatengeneza wataalamu wenye ubora kwa ajili ya kuwasaidia watanzaina.

Naye Katibu wa  Chama Cha Walimu Tanzania (CWT), Deus Seif amesema kuwa bila kuwa na walimu wenye ubora katika Shule wataendelea kuzalisha watalaamu wasio na vigezo hivyo walimu wanapaswa kutoa elimu yenye vigezo vya kutosha ili kusaidia taaluma hiyo inayotegemewa na taifa.

"Niwahakikishie mwalimu akikosea gharama yake ni kubwa sana kuliko kosa la kufanywa na daktari au Mhandisi kwa sababu unaweza kulirekebisha lakini kosa la mwalimu ni hatari sana,"Amesema Deus Seif






Post a Comment

0 Comments

TAWA YAPOKEA TUZO KUTOKA KWA TAASISI YA FOUNDATION FOR DISABILITIES HOPE (FDH)