Na Immaculate Dodoma
WAKALA ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) umewataka wavumbuzi kulinda bunifu zao kisheria kwa kuzisajili kwa Wakala na kuziwekea linzi.
Hayo alisema Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Miliki Bunifu wa BRELA, Seka Kasera kwenye Maonesho ya Wiki ya Ubunifu yanayoendelea Jijini hapa.
Maadhimisho ya Wiki ya Ubunifu yaliyoanza juzi jijini hapa yanakwenda sambamba na Mashindano ya Kitaifa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu(MAKISATU).
Aidha alisema ni vyema kwa wavumbuzi kuhakikisha wanasajili ulinzi wa bunifu zao kisheria kwa kusajili bidhaa zao kwa wakala wa BRELA.
Alisema baada ya kupita kwenye mabada wamebaini kuwapo kwa bunifu nyingi zenasifa ya kupata linzi ambazo zimebuniwa na vijana wadogo na ambazo zikipata linzi itaweza kupata soko la kitaifa na kimataifa
" Tumeweza kupitia baadhi ya mabanda kuangalia zile bunifu na ambazo zimepata ulinzi kutokana na kuwa tumezisajili, lakini pia zipo bunifu nyingi zinasifa ya kupata linzi na tena ni za vijana wadogo sana lakini wamefanya bunifu ambazo zikipata linzi itaweza kupata soko la kitaifa na Kimataifa."
" Tunachofanya Sasa kwenye haya maonesho tunawashauri waje kupata linzi kwa bunifu ambazo hazijasajiliwa kwa maana ya kupata linzi za kisheria maana tunaona zinasifa za kupata linzi."
Aidha, Kasera pia ametoa rai kwa wabunifu ambao wamesajili bunifu zao kuendelea kuziboresha kulingana na mahitaji ya jamii ili ziwe na tija zaidi.
" Kwa zile bunifu zilizosajiliwa wasiachie pale pale waende kama kaulimbiu inavyosema mendeleo endelevu wajaribu kuziboresha kwa kadri mahitaji ya jamii yanavyohitaji.
" Tangu mwaka 2019, China inaongoza kwa kutoa bunifu nyingi lakini haiongozi kwa kutoa bunifu mpya bali inaongeza kwa kuziongezea ubora bunifu za zamani, mfano kama amebuni simu wanachofanya ni kufanya maboresho zaidi kwenye hiyo simu.
" Tunamshauri aangalie namna gani anaweza akaboresha ile bunifu yake, hivyo kile atakachokuja kufanya ni kuongeza ubora wa ile bunifu
Kwa mfano ubunifu ya gari miaka yote gari ipo lakini siku zinavyokwenda wanatoa matoleo mapya yenye ubora zaidi, ulinzi zaidi, uharaka zaidi na sisi tumekuwa tukitoa elimu ya namna gani wanaweza wakaboresha zile bunifu zao ambazo kimesajiliwa."
Aidha, Kasera alisema BRELA inaangalia namna ambayo wanaweza kushirikisha taasisi zingine katika kusaidia kuzipatia soko kwa bunifu hizo
" Kuna mtu ana bunifu nzuri lakini awezi kuzipatia soko kwa hiyo BRELA na taasisi zaingie za kikanda na Kimataifa tumekuwa tukiangalia zile zinahitaji msaada wetu kuzitafutia soko."
Kasera alisema Wakala itaendelea kupita kwenye mabada na kuzungumza nao kuwa hii inaweza kupata ulinzi au ongeza ubora wa bunifu zao.
Pia ametoa Rai kwa wanadosoma kutumia maonesho hayo kupata elimu na huduma ya kusajili kampuni, leseni za biashara kundi A na viwanda sambamba na kutoa ulizi wa bunifu hapo hapo uwanjani.
0 Comments