MBUNIFU WA KIKE WA DIT ANG'ARA MAKISATU 2022

Mbunifu wa  kifaa chakupumulia watoto waliozaliwa na shida ya upumuaji (Bubble CPAP Machine
 Machine), Sandra Sommi ambaye amebuni Kifaa Tiba cha kutatua changamoto ya watoto wachanga katika upumuaji  wenye umri chini ya mwezi mmoja hasa waliozaliwa  njiti akifurahia zawadi ya ushindi  ya Hindi ya milioni tano aliyokabidhiwa katika maonyesho ya wiki ya ubunifu yanayokwenda sambamba na Mashindano ya Ubunifu wa Sayansi na Teknolojia( MAKISATU), kwa mwaka 2022
Na Asha Mwakyonde,DodomaT

TAASISI ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT),imekuwa  mshindi wa kwanza katika maonyesho ya wiki ya ubunifu yanayokwenda sambamba na Mashindano ya Ubunifu wa Sayansi na Teknolojia( MAKISATU), kwa mwaka 2022, kupitia Mbunifu wake Mhandisi wa Kompyuta Sandra Sommi ambaye amebuni Kifaa Tiba cha kutatua changamoto ya watoto wachanga katika upumuaji  wenye umri chini ya mwezi mmoja hasa waliozaliwa  njiti (Bubble CPAP Machine Machine).

Maonyesho hayo  yameendaliwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Kimataifa la Mpango wa Maendeleo (UNDP),kupitia mradi wake wa FUNGUO, yanayomalizika  katika viwanja vya Jamuhuri jijini hapa.

Akizungumza jana Mei 19,2022, jijini hapa katika viwanja vya jamuhuri mara baada ya ushindi huo Sandra amesama kuwa lengo la kubuni kifaa hicho ni kutatua changamoto kwa watoto wachanga wengine wanazaliwa na tatizo la upumuaji.

Sandra ameeleza kuwa  wazo la kutengeneza mradi wa kifaa hicho cha mashine  lilitoka kwa baadhi ya madaktari kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili(MNH),walipokuwa wakufanya mafunzo yao (Field), waliwapa changamoto ya kutengeneza vifaa ambavyo wanavitumia wakiwa katika mafunzo hayo.

Ameongeza kuwa mradi huo umelenga kupunguza gharama za ununuzi wa mashine za kumpumulia watoto hao ambapo vikiagizwa kutoka nje ya nchi ni gharama kubwa na kwamba nchini Malawi mashine hiyo ndio wanaouza kwa bei nafuu kidogo zaidi ya milioni 4.

"Tulivyorudi chouni tulitengeneza kifaa tiba cha kwanza ambacho kinafanya kazi lakini changamoto yake hewa inapitia hapa (anaonyeshea) inaweza ikamsababisia mtoto kupoteza maisha baada ya kukupeleka Muhimbili tuliambiwa tukiboreshe," amesema Mbunifu huyo.

Sandra amesema kuwa baada ya kupata maoni alitengeneza kifaa cha pili ambacho alikiboresha kwa kuweka unyevu unyevu sehemu ya kupumulia mtoto na hadi kukamilika kimegharimu laki nane( 800,000) tofauti na kile cha kwanza ambacho kiligharimu laki nne(400,000).

Amefafanua kuwa kifaa tiba hicho kikitoka nje ya nchi kinauza  zaidi ya milioni 1.5 na utengenezaji wake umechukua mwezi mmoja hadi kukamilika.

"Nimekuja hapa na ubunifu ambao unahusu kifaa tiba kwa ajili ya watoto chini ya umri wa mwezi mmoja wenye changamoto ya kupumua unaweza kukuta mtoto mara baada ya kuzaliwa anakuwa na shida ya upumuaji anaweza kuwa chini ya siku tano kifaa hiki kinasaudia," amesema.

Akizungumzia ushindi huo Mkuu wa taasisi hiyo  Profesa Preksedis Ndomba amesema kuwa wamefurahia ushindi alioupata Sandra kwa niaba ya DIT ambao unatokana na miundombinu ambayo wameiweka.

Prof.Ndomba amesema kuwa Sandra ametoka katika Maabara ya Design Studio yenye lengo la kuimarisha ubunifu wa wanafunzi wao kwani wanachojifunza darasani wakienda kwenye mabara hiyo wanajifunza kwa vitendo.

" Sandra ni kati ya wengi aliamua kukaa na kuunda kifaa hiki, watoto wengi wanapoteza maisha kwa kukosa mashine hii, baadhi ya Hospitali ikiwamo Muhimbili walivutiwa na ubunifu wa kifaa tiba hiki," amesema Prof. Ndomba.

Amesema tayari kifaa hicho kimeshafanyiwa majaribio ya awali hivyo wanajiandaa kusheherekea ushindi huo na kwamba wameshaanza kumuendeleza kimasomo Mbunifu huyo.


Post a Comment

0 Comments

 KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA, KATIBA NA SHERIA YANOLEWA